Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiweka saini kitabu cha maombolezo leo ikulu ya Addis Ababa kufuatia
kifo cha Waziri Mkuu wa Ethiopia Marehemu Meles Zenawi anayetarajiwa kuzikwa
kesho.
Wengine katika picha
ni baadhi ya wajumbe waliofuatana na Rais Kikwete watakoshiriki mazishi ya
kiongozi huyo. Kutoka kushoto ni Mbunge wa
Mtera Mhe.Livingstone Lusinde, Aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Ethiopia
Jenerali Mirisho Sarakikya, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe.Joram
Boswaro, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe.Zitto Kabwe na Waziri wa Kazi wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua na kutoa heshima zake mwisho
kwa aliyekuwa Waziri mkuu wa Ethiopia Marehemu Meles Zenawi katika
Ikulu ya Addis Ababa jioni hii
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akito heshima zake mwisho kwa aliyekuwa Waziri mkuu wa Ethiopia Marehemu Meles Zenawi
katika ikulu ya Addis Ababa jioni hii
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akikutana na kufanya
mazungumzo na Kaimu Waziri MKuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn jijini Addis Ababa jioni hii.
No comments:
Post a Comment