Serikali
ya Marekani imetoa msaada wa kuimarisha Mfumo wa Ulinzi baharini wenye thamani
ya dola za Marekani milioni 1 ikiwa ni mafunzo pamoja na vifaa.
Balozi wa
Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt ameshiriki katika hafla ya kukata
utepe wa kufungua mafunzo pamoja na msaada huo katika kambi ya Kigamboni
Wanamaji wa Kigamboni ya TPDF jijini Dar es Salaam.
Msaada
huo kwa ujumla utasaidia ushirikiano wa kupata taarifa miongoni mwa Mamlaka za
Bandari, askari wa majini na Jeshi la Wananchi wa Tanzania ikiwa ni kuongeza
usalama majini.
No comments:
Post a Comment