Ripoti ya Umoja wa mataifa iliyofichuliwa
inasema wanajeshi kutoka Rwanda walihusika moja kwa moja na utekaji wa mji wa
Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo uliotekelezwa na waasi.
Ripoti
hiyo iliyokusanywa kwa ajili ya baraza la usalama, inasema wanajeshi mia tano
wa Rwanda, walihusika katika utekaji huo wa kundi la M23.
Msemaji
mmoja wa jeshi la Rwanda ameiambia BBC kuwa tuhuma hizo ni za kuudhi na zisizo
na msingi.
Wanajeshi
wa Congo walirudi Goma hapo jana siku mbili baada ya waasi kuondoka kutoka mji
huo wa Goma mwishoni mwa wiki baada ya mkataba wa amani uliofikiwa kwa usaidizi
wa nchi za ukanda wa Maziwa Makuu.
Lakini
waasi wameonya kuwa watauteka tena mji huo ikiwa serikali haitatimiza matakwa
yao katika muda wa siku mbili.
Waasi
hao waliondoka Goma siku kumi na moja baada ya kuuteka mji huo kutoka kwa
wanajeshi wa DRC wakiungwa mkono na wanajeshi wa amani wa Umoja wa Mataifa
Mnamo
Jumatatu mamia ya wanajeshi wa DRC waliwasili katika kambi zao mjini Goma baada
ya waasi kuondoka kutoka mji huo mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini siku ya
Jumamosi.
Jean-Marie Runinga (Katikati) ni
kiongozi wa kisiasa wa M23
|
Uwanja
wa ndege wa mji huo utafunguliwa Alhamisi ili kuruhusu misaada ya kibinadamu
kuingizwa huko kuwasaidia mamia ya watu walioachwa bila makao baada ya kutoroka
mapigano.
Waasi
hao walikubali kusonga umbali wa kilomita 20 kutoka Goma ikiwa serikali
itatimiza matakwa yao ikiwemo kuwaachilia wafungwa wa kisiasa. Lakini duru
zinseama kuwa wangali wako karibu sana na mji wenyewe kinyume na makubaliano
walioafia.
Kuna
hofu kuwa hatua yao isidumu ikiwa Rais Joseph Kabila atakataa kuanza mazungumzo
nao kulingana na msemaji wa waasi hao kanali Vianney Kazarama.
No comments:
Post a Comment