Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Chuo cha UIinzi (National
Defence College) Jana Septemba 10, 2012 Kunduchi jijini Dar es salaam. Kulia
kwake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na kushoto kwake
ni Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makalala na kushoto kabisa ni
aBalozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu Younqing.
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akipeana mikono na Mkuu wa Chuo cha UIinzi (National Defence College)
Meja Jenerali Charles Makalala Jana Septemba 10, 2012 baada ya kumkabidhi mfano
wa funguo kama ishara ya kufungua rasmi chuo hicho kilichopo Kunduchi jijini
Dar-es-Salaam. Kulia ni Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange.
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akiwa na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi (National Defence College) Meja
Jenerali Charles Makalala baada ya kufungua rasmi chuo hicho kilichopo Kunduchi
jijini Dar-es-Salaam, nyuma yao ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
Mhe. Shamsi Vuai Nahodha anayefuatana na mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali
Davis Mwamunyange
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisoma hotuba yake kufungua rasmi Chuo cha ulinzi
(National Defence College) kilichopo Kunduchi jijini Dar-es-Salaam, pamoja na
kuzindua kozi ya kwanza ya mwaka mmoja.
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akipozi kwa picha ya pamoja na wanachuo wa kozi ya kwanza ya mwaka
mmoja katika chuo cha ulinzi alichofungua rasmi hapo jana septemba 10, 2012
Kunduchi jijini Dar-es-Salaam.
Picha kwa hisani ya: IKULU
No comments:
Post a Comment