HALMASHAURI
Kuu ya CCM (NEC),
imetangaza majina ya wagombea walioteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi
ndani ya chama hicho, huku ikionyesha kuwa uchaguzi huo utakuwa na mchuano
mkali.
Katika orodha iliyotolewa jana, baadhi ya makada wake maarufu akiwamo Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na Salum Londa wametupwa.
Katika orodha iliyotolewa jana, baadhi ya makada wake maarufu akiwamo Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na Salum Londa wametupwa.
Mchuano
mkali unaonekana kuwapo kwenye nafasi ya ujumbe wa Nec Mkoa wa Manyara ambako
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye anachuana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu.
Mchuano
huo unatarajiwa kuwa mkali katika nafasi ya uenyekiti kwenye baadhi ya mikoa
kutokana na kupitishwa kwa majina ya makada wake maarufu. Mwanza ni miongoni
mwa mikoa hiyo kwani Nec imepitisha jina la Waziri wa zamani wa Maliasili na
Utalii, Anthony Diallo ambaye atachuana na Clement Mabina anayetetea nafasi hiyo.
Makada
hao watapata ushindani mkali kutoka kwa Zebedayo Athumani, Joseph Yaredi na
Mashimba Hussein Mashimba.
Dar
es Salaam nako kunatarajiwa kuwa na mchuano mkali kwani mwenyekiti wa sasa,
John Guninita atachuana na Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi Makao Makuu ya CCM,
Matson Chizzi na kada mwingine, Ramadhan Madabida. Godfrey Mwalusamba, Harold
Adamson na Paul Laizer wanawania nafasi hiyo mkoani Arusha.
Katika
Jumuiya ya Wanawake wa Tanzania (UWT), ambako Mwenyekiti wa sasa, Sofia
Simba ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto anachuana na
Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango Malecela na Mbunge wa Viti Maalumu,
Mayrose Majige.
Awali,
Mkono alikatwa jina lake na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo na kutangaza
hali ya hatari akisema asipopitishwa patachimbika. Jina lake lilirejeshwa na
Kamati ya Usalama na Maadili kabla ya kukatwa tena na Kamati Kuu.
Alipoulizwa
jana kuhusu kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho, Mkono alisema:
“Nimekubaliana na uamuzi wa chama na nitaendelea kuwa mwanachama wa CCM.
Nimelelewa na kukulia CCM na nitaendelea kubaki CCM nikiwa mwanachama mtiifu.”
Katika
Jumuiya ya Vijana (UVCCM), mchuano mkali unaonekana kuwa katika
nafasi ya makamu mwenyekiti kwani mmoja wa wagombea waliopitishwa, Paul Makonda
anaaminika kuwa na nguvu kubwa kutoka katika kundi la wabunge na mawaziri
wapambanaji wa ufisadi. Makonda anawania nafasi hiyo pamoja na Mboni Mhita na
Ally Hapi.
Nafasi
ya Mwenyekiti UVCCM inawaniwa na Sadifa Juma Khamis, Rashid Simai Msaraka na
Lulu Mshamu Abdallah.
Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa atachuana na Dk Salash Toure na Nanai Kanina kwenye nafasi ya ujumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Monduli.
Vigogo kadhaa wamepitishwa kuwania nafasi 10 za Nec, wakiwamo baadhi ya mawaziri na viongozi wa juu wa chama hicho.
Miongoni
mwao ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, Waziri wa
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo David, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, Naibu Waziri wa Sayansi na
Teknolojia, January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Benard Membe na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama.
Wengine
ni Katibu wa Fedha na Uchumi CCM, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Uhusiano, Stephen Wassira, Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na
Vijana, Dk Fenela Mukangara na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela.
Kwa
upande wa Zanzibar,
nafasi 10 za Nec kupitia kapu zinawaniwa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif
Ali Iddi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan.
Katika
orodha hiyo wamo, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi, Waziri wa zamani
wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Mohamed Seif Khatib, Waziri wa Fedha na
Mipango wa Zanzibar, Omar Yussuf Mzee na Naibu Waziri wa Fedha wa zamani,
Abdisalami Issa Khatib.
Katika uteuzi huo wa wagombea, majina matatu ya wagombea kutoka katika familia ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete yamepitishwa.
Katika uteuzi huo wa wagombea, majina matatu ya wagombea kutoka katika familia ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete yamepitishwa.
Waliopitishwa ni
pamoja na mkewe Salma Kikwete ambaye anakuwa mgombea pekee katika nafasi ya
ujumbe wa Nec Lindi Mjini na Ridhiwan Kikwete ambaye pia ni mgombea pekee wa
nafasi hiyo katika Wilaya ya Bagamoyo.
Mbali ya hao, Nec pia
imepitisha jina la Mohamed Mrisho Kikwete kuwania nafasi ya uenyekiti wa Wilaya
ya Bagamoyo.
Vigogo watemwa
Nec imewatema vigogo kadhaa, baadhi yao ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Azim Premji na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Vicky Nsilo-Swai ambaye alikuwa anagombea ujumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Hai na kada wa siku nyingi, Salum Londa.
Vigogo watemwa
Nec imewatema vigogo kadhaa, baadhi yao ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Azim Premji na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Vicky Nsilo-Swai ambaye alikuwa anagombea ujumbe wa Nec kupitia Wilaya ya Hai na kada wa siku nyingi, Salum Londa.
Pia
wamo wabunge, Sarah Msafiri, Munde Tambwe, Deo Filikunjombe na Victor
Mwambalaswa.Wengine waliotemwa ni Hussein Bashe na hasimu wake mkubwa kisiasa
Dk Hamis Kigwangalla, Jamali Kassim, Anthony Mavunde na Emmanuel Nzungu, ambaye
aliomba kugombea Uenyekiti Wilaya ya Ilemela, Mwanza.
No comments:
Post a Comment