Mtuhumiwa
wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel
Ten Daud Mwangosi leo amefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi
ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili.Huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa
askari.
Akisomewa
shitaka lake na mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu lilian ngilangwa ,
amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace
Simoni (23) mkazi wa FFU Iringa, anakabiliwa na shitakala la mauaji ya
makusudi.
Amesema
mtuhumiwa huyo mnamo 02 Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya
Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu
cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.
Mbele
ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo
mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi
kusikiliza kesi za mauaji.
Kwa
mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16
iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia
kupewa dhamana.
Mtuhumiwa
amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo
imeahirishwa hadi 10 Oktoba mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Hata
hivyo askari wengi waliompeleka mtuhumiwa huyo wakiwa wamevaa nguo za kiraia
walihakikisha kuwa mtuhumiwa huyo hapigwi picha jambo ambalo limewaletea ugumu
waandishi waliokuwapo baada ya kusukumwa ovyo kuzuia mtuhumiwa huyo asipigwe
picha.
Kila
wakati waandishi walipotaka kupika picha walikuwa wakisukumwa na askari hao
huku mtuhumiwa akiwa amejifunika kichwa na kuvaa miwani meusi kuhakikisha kuwa
sura yake haionekani na waandishi hao.
Katika
hali isiyo ya kawaida mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo kwa gari
binafsi la kifahari lenye namba za usajili DFP 2175 Toyota Land cruiser tofauti
na watuhumiwa wengine ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa gari la polisi.
No comments:
Post a Comment