Mhe.
Kattikiro akiwa jukwaani akinadi sera za chama chake
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Ukonga jana kiliendeleza kile kilichokiita
Mwendelezo wa uvunja na kuibomoa ng’ome ya CCM jimboni humo, katika harakati
zake za kukiimarisha chama zaidi kwa operations zake za M4C.
Katika
mkutano huo wa hadhara uliofanyika viwanja vya mzambarauni, mgeni rasmi
aitegemewa kuwa Mhe. Joshua Nassari (MB), lakini hakuweza kutokea kutokana na
kuwa na kikao cha Kamati Kuu ya Chama hapo jana. Hivyo basi wapambanaji wengine
walishika nafasi hiyo ya kuendesha vuguvugu hilo la mabadiliko ambapo Diwani wa
Viti maalumu, Mhe. Grace Shellukindo, Mhe. Maxmillian Kattikiro, Mwk. Wa Chadema
Jimbo ndg. Michael Aweda, Katibu wa Jimbo ndg. Mwaipopo, Mwk. Wa Kamati ya
Wahanga wa Mabomu G/mboto ndg. Obadia, aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la mvomelo
ndg. Matokeo, Advocate Nixon, Mwk. Wa Bavicha Jimbo, ndg. Fredrick Kabati na
wengine wengi walikuwepo ili kuweza kuisambaratisha vilivyo ngome hiyo ya CCM
ambapo walifaulu kwa kiasi kikubwa sana.
Akiongea
katika mkutano huo Mhe. Kattikiro aliwataka CCM kuacha siasa chafu za
kuchafuana zinazoendelezwa hivi sasa na watawala wetu na kusisitiza ni vyema
watawala wakajikita zaidi katika kutafuta ufumbuzi juu ya kuwakwamua Watanzania
toka katika wimbi kubwa la umasikini walilonalo.
Aidha
aliongeza kuwa, Tanzania ni nchi tajiri kuliko zote duniani, lakini utajiri
wake umekuwa ukiwanufaisha watu wachache wenye madaraka na wageni ambao
huingizwa nchini kwa kofia ya uwekezaji.
Akitoa
mifano kadhaa, alinukuu kauli ya Mheshimiwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame kuwa, “kama
nchi yangu ingepewa bandari hii ya Dar-es-Salaam pekee, basi ningeweza kuifanya
Rwanda moja ya mataifa tajiri mno duniani” hivyo alihoji je Tanzania
tunabandari ngapi? Mtwara, Tanga, Zanzibar na Dar-es-Salaam, Je viongozi wetu
hawana mawazo ya nini kifanyike kwa kutumia raslimali hiyo ya bandari kuweza
kuinua uchumi wetu? Au vichwa vyao (Viongozi) vinautofauti gani na kichwa cha
Kagame kuwa yeye awe na uwezo huo lakini watanzania tusiwe nao? Alihoji.
Alisema,
“Kauli ya Kagame, ilikuwa ikituambia watanzania kuwa, viongozi wenu
mliowachagua (CCM) hawana nia ya dhati ya kuwakwamua toka kwenye umaskini
uliowagubika watanzania, wako kwa ajili ya manufaa yao binafsi na ndiyo maana
wameshindwa kutumia fursa mbalimbali za raslimali kemkem ambazo Tanzania
imetunukiwa na Mwenyezi Mungu bure”.
Katika
Mkutano huo wa hadara CHADEMA ilikuwa inawakaribisha wanachama wapatao 46 toka
CCM na vyama vingine vya upinzani ambapo walisarimisha kadi zao kwa Mwenyekiti
wa Jimbo Mhe. Aweda naye kuwakabidhi kadi ya chama hicho.
Awada
aliwapongeza sana makambanda hao wapya, ambao wameamua kishujaa kikihama chama
tawala (Kuvua Gamba) na kuhamia chadema (Kuvaa Gwanda).
Akizungumza
kwa niaba ya wanaCCM ambao walijisalimisha kikamilifu kwa makamanda hao wa
CHADEMA ambao walikuwa wakiendesha oparesheni hiyo, aliyekuwa Mwenyekiti wa
Vijana wa CCM, alisema,
“Tunawashukuru
sana wanaCHADEMA kwa kutukaribisha CHADEMA, kwani CCM hakuna jipya ambalo sisi
ambao tulikuwa wanachama wake tunaweza kulisema na kulisimamia. Kikubwa ambacho
tumekiona huko (CCM) ni ufisadi na ubadhilifu wa mali za umma, wamekuwa
wakijinufaisha wenyewe huku sisi wananchi tukibaki maskini siku hadi siku”.
Hivyo aliwataka wanaCCM wengine ambao bado
wanasitasita kukiunga mkono CHADEMA, wajitokeze na wasihofie mafisadi, kwani
hawana nafasi tena katika nchi hii, kwani kwa miaka 50 ya utawala wao hakuna
uwiano na maendeleo yaliyo fanyika kulinganisha na raslimali tulizonazo.
Habari katika Picha zaidi tafadhali bofya hapa.....
Kamanda Kattikiro akitoa maelekezo fulani katika mkutano huo
Viongozi wa Jimbo wakibadilishana mawazo
Mshereheshi wa mkutano wa hadhara wa CHADEMA ndg. Ramadhani Mgaya akiwa kazini
Poweeeeer .... kama ionekanavyo makambanda wakiitikia salamu
Baadhi ya Viongozi wa Chadema ngazi ya Jimbo wakiwa wanfuatilia kwa ukaribu toka kwa msemaji.
Sehemu ya Wananchi na wanachama wa CHADEMA waliojitokea kusikiza makamuzi hapo jana.
Mhe. Grace Shellukindo, Diwani wa Viti Maalum, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala akifunguka.
Katibu Mkuu wa Jimbo la Ukonga Mhe. Mwaipopo akimwaga sera za kuwaponda mafisadi.
Mwenyekiti wa jimbo, Mhe. Michael Aweda, naye hakubaki nyuma kuungana na wenzake kuisambaratisha CCM
Waliokuwa wanachama wa CCM, wakipokelewa na Mwenyekiti wa Jimbo, pia
wakikabidhi vilivyokuwa vielelezo vyao vya U-CCM kwa chama hicho huku
wakishuhudiwa na watu.
Tukibadilishana mawazo wakati wa mkutano huo na Advocate Nixon, juu ya mambo kadha wa kadha.
No comments:
Post a Comment