Waasi wa Kundi la M23 |
Mkuu
wa harakati za kudumisha amani wa Umoja wa mataifa Herve Ladsous ameliambia
baraza la usalama la Umoja huo kwamba waasi wameidhinisha kile anachokiita kuwa
ni utawala wa kimabavu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Bwana
Ladsous amesema waasi wa M23 wanadhibiti idadi kubwa ya maeneo ya Mashariki mwa
Congo na wanawatoza kodi wananchi .
Taarifa zinazohusiana
Umoja
wa Mataifa unaishutumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23. Wakati huo huo
Maafisa wa Congo wanataka Rwanda iwekewe vikwazo biashara ya madini .
Waziri
wa Madini wa Congo, ameziandikia nchi za Marekani na Uingereza akizitolea wito
kampuni katika nchi hizo ziache kununua madini kutoka Rwanda, ambayo mengi
anasema yanachimbwa katika ardhi ya Congo.
Zaidi
ya watu 200,000 wameachwa bila makao kufuatia mapigano Mashariki mwa nchi.
Mkutano
wa maafisa wa ngazi ya juu watakaojadili mzozo huo unatarajiwa kufanyika katika
baraza la usalama la Umoja wa mataifa mjini New York wiki ijayo.
"waasi
wa M23 wako katika pembe moja ya mkoa wa Kivu Mashariki ambao unapakana na
Rwanda na Uganda'' alisema bwana Ladsous wakati akiwahutubia waandishi wa
habari mjini New York.
Wananchi wa Congo wanaokimbia vita |
"ni
kama ambao wanatawala kwani wanawatoza kodi wenyeji wa mkoa huo , jambo hili
halikubaliki hata kidogo'' aliongeza bwana Ladsous.
Wakati
huohuo, maafisa wa utawala nchini DRC wanataka vikwazo kuwekewa biashara ya
madini yanayotoka nchini Rwanda.
Wadadisi
wanasema kuwa madini mengi yanayotoka nchini Rwanda huenda yalitoka nchini DRC
na kuchimbwa na makundi ya waasi walio na uhusiano na Rwanda.
"namna
tunavyoweza kukomesha kabisa mzozo huu ni Rwanda kuwekewa vikwazo vya
kibiashara kwa madini yanayotoka nchini humo hadi tutakapoweza kupata suluhu la
kudumu kwa mzozo katika mikoa ya Kaskazini na Kusini ma Kivu.'' alisema waziri
wa madini wa DRC Martin Kabwelulu. .
Taarifa kwa hisani ya BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment