Waziri Mbarawa akitoa hutoba.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Six Telecoms, Rashid Shamte akitoa mada
katika mkutano wa capacity Africa.
Naibu Waziri, January
Makamba na Mkurugenzi Mkuu wa Six Telecoms, Rashid Shame akiwa na Mkuu wa
kampuni ya Main One Cable Fun
======== ======== ========
Serikali imesema itatumia shs 30 bilioni
kukamilisha ujenzi wa mkongo wa taifa na kurahisisha huduma hiyo hapa nchini.
Hayo yalisemwa na Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Technolijia, Makame Mbarawa
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa sita wa wadau wa mawasiliano duniani (Capacity
Africa) uliodhaminiwa na kampuni ya Six Telecoms ambao umefanyika Tanzania kwa
mara ya kwanza kwa siku mbili.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Six Telecoms, Rashid
Shamte alisema ujio wa mkongo wa taifa utawavutia zaidi wawekezaji kuja
Tanzania kuwekeza kwenye sekta hiyo. Shamte alisema lengo la mkutano huo ni
kuitumia Tanzania kuwa njia ya mawasiliano kwa nchi nane ilizopakana nazo na
kuongeza kwamba hiyo itasaidia pia kupunguza gharama kwa watumiaji wa sekta ya
mawasiliano hapa nchini.
Alisema kuwa wamefarika sana kufanikisha mkutano
huo na kutambulisha mtandao wao wa Metro ambao unaongoza katika soko kwa hivi
sasa. Kwa mujibu wa Shamte, pamoja na changamoto kadhaa wanazokabiliana nazo, wameweza
kujidhatiti ili kuweza kufikia lengo lao hapa nchini na katika makampuni
mengine nje ya Tanzania yanayotumia huduma yao.
“Ninafuraha kubwa kuona mkutano huu wa Capacity
Africa unafanyika hapa nchini na mwitikio kuwa mkubwa, kwa kweli hii ni faraja
sana kwetu, najua mkutano huu utatoa picha ya nini kitafanyika ili kukabiliana
na changamoto ambazo watumiaji wa huduma zetu wanakabiliana nazo, naipongeza
serikali kwa kutoa sapoti kubwa na wadau wote duniani kukutana na hili ni kwa
ajili ya kujenga na kuleta maendeleo katika nchi zetu,” alisema Shamte.
Wadau wa mawasiliano zaidi ya 350 kutoka nchi 50
duniani ulilenga pia kuitumia Tanzania kuwa njia kuu ya mawasiliano kwa nchi
nane za Afrika. Shamte alisema ujio wa mkongo wa taifa utawavutia zaidi wawekezaji
kuja Tanzania kuwekeza kwenye sekta hiyo. Alisema kuwa lengo la mkutano huo ni
kuitumia Tanzania kuwa njia ya mawasiliano kwa nchi nane ilizopakana nazo na
kuongeza kwamba hiyo itasaidia pia kupunguza gharama kwa watumiaji wa sekta ya
mawasiliano hapa nchini.
Wadau wengine waliodhulia mkutano huo ni
wawakilishi kutokaLiquid Telecom, WIOCC, Safaricom Business, Seacom, Gateway na
kampuni mbalimbali za mawasiliano duniani.
No comments:
Post a Comment