Hivi ndivyo
mkazi wa Wenda alivyochunwa ngozi na watu
wasiojulikana (Tunaomba Radhi kwa picha hizi
)
Eneo
la tukio
Hivi karibuni vyombo vya habari viliripoti tukio
la kusikitisha linalohusisha mauaji ya kinyama ya dereva wa bodaboda Sadiki Mbelwa
(26) katika kijiji cha wenda, Tanangozi Iringa ambapo mwili wa marehemu
ulikutwa ukiwa na majeraha sehemu za kichwani huku ikisadikiwa kupigwa na kitu
chenye ncha kali.
Leo katika tukio lingine la kusikitisha ambalo limetokea katika kijiji cha
wenda kitongoji cha Lupeta umekutwa mwili mwanakijiji aliyetambulika kwa jina
la Leornad Kutika (49).
Mwili wa marehemu Kutika umekutwa katika nyumba aliyokuwa akiishi huku ukiwa
umechunwa ngozi, kunyofolewa macho pamoja na kukatwa sehemu za siri.
Akiongea na vyanzo vya habari hizi kwa huzuni baba mdogo wa marehemu Martin
Kutika mkazi wa lupeta anaeleza kuwa usiku wa kuamkia jana alipigiwa simu ndugu
wa marehemu aliyefahamika kwa jina Kibadeni kutika kuwa ndugu yake huyo ambaye kwa
mujibu wa maelezo yake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la akili alikutwa katika
nyumba aliyokuwa anaishi huku akiwa amefariki na kuondolewa sehemu za siri na
kuchunwa ngozi. Zawadi Mwenga ambaye pia ni ndugu wa marehemu anaeleza kuwa
alipata taarifa za tukio hilo jana na ndipo alipofika katika nyumba ya marehemu
na kukuta akiwa amefariki.
Akilelezea kuhusu tatizo alilokuwa nalo marehemu Mwenga amesema marehemu
alianza kusumbuliwa na tatizo la kurukwa akili tangu alipokuwa mdogo japo
hakuwahi kufanya vurugu yoyote na wao kama familia wamekuwa wakimpatia chakula
na siku mbili kabla ya tukio marehemu alionekana lakini baada ya hapo
hawakumuona tena ndipo wifi yake alipofika nakukuta marehemu amekufa huku akiwa
ametendewa unyama huo.
Afisa mtendaji wa kijiji cha wenda Dismas Ngweta anaeleza kuwa alipigiwa simu na mwenyekiti wa kjjij cha lupeta Geofrey Dugange na kumweleza kuwa hakuna amani katika kijiji hicho kuwa kuna mwanankijiji ambaye ameuawa.
Akielezea baada ya kufika eneo la tukio Ngweta anaeleza kuwa walipouangalia mwili wa marehemu waligundua kuwa amechunwa ngozi, kunyofolewa macho, kukatwa sehemu za siri pamoja na kutobolewa katika sehemu ya mguu. Akilinganisha tukio hili na lililotokea siku chache zilizopita Ngweta ameeleza kuwa tukio la dereva wa bodaboda limetokea wakati wa usiku na kusema kuwa inasemekana kuwa tukio la pili limetendeka usiku kwani kwa mujibu wa wanakiji walieleza kumwona marehemu jioni kabla ya tukio.
Je nijuhudi gani zimefanywa na jeshi la polisi mpaka sasa? Ngweta ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hilo alipiga simu kwa mkuu wa kituo cha Ifunda naye akajibu kuwa anawasiliana na kituo kikubwa Iringa. Mpaka vyanzo vyetu vya habari vinatoka eneo la tukio hakuna afisa usalama aliyekuwa amefika katika eneo hilo.
Tukio hili ni la mara ya pili kutokea baada ya tarehe 25 Septemba 2012, kuripotiwa kuuwawa kinyama kwa dereva wa bodaboda na pikipiki yake kutoonekana.
No comments:
Post a Comment