Mhe. Hamad Rashid Mohamed (CUF) |
MBUNGE
wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), amelaani matumizi ya nguvu za Jeshi la
Polisi wakati wa chaguzi mbalimbali huku akikishauri chama chake kujiondoa
katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa baina yao na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kutokana na kutowasaidia wananchi.
Akizungumza
na Tanzania Daima kwa njia ya simu, Hamad alisema kuwa ameshangazwa na nguvu
kubwa ya Jeshi la Polisi iliyotumika katika uchaguzi mdogo wa Bububu
uliomalizika hivi karibuni na hivyo kusababisha kujeruhi wananchi bila sababu.
Alisema
CUF iliingia katika serikali ya mseto kwa lengo la kuweka uhuru na haki lakini
wameshindwa kufikia azima hiyo na kwamba ikiwa muafaka huo ni kwa maslahi ya
watu wachache basi wajitoe.
“Mimi
nashangaa sana hayo mazungumzo sijui yalikuwa ya nini na ‘ndoa’ ilikuwa ya nini
kama ilikuwa ni kwa masilahi ya watu wachache huku wananchi hawanufaiki nayo,
wanapigwa risasi, basi CUF wajiondoe kama si kwa masilahi ya wananchi wote,”
alisema Hamad.
Hata
hivyo, Hamad alisema Serikali ya Zanzibar inaundwa na vyama viwili, hivyo ni
dhahiri kwamba CCM na CUF ndio wametumia nguvu katika kuvikandamiza na kuhujumu
vyama vidogo vya siasa ambavyo havikuwa na serikali.
Katika
uchaguzi huo wa Jumapili ambao CCM iliibuka kidedea ikifuatiwa na CUF na Chama
kipya cha ADC, vurugu kubwa zilizuka huku matokeo hayo yakipingwa vikali.
Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment