ADAI NI KWA
KUWAPITISHA WATUHUMIWA WA UFISADI KUGOMBEA
Katibu Mkuu Chadema, Dr. Willibroad Slaa |
KATIBU
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa,
amemvaa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, akisema
amekitengenezea kaburi la kukizika rasmi chama chake kwa kuruhusu watuhumiwa
wakubwa wa ufisadi kugombea nyadhifa mbalimbali.
Dk.
Slaa alisema uteuzi wa wagombea ndani ya CCM uliomalizika juzi umeonyesha wazi
kwamba sasa chama hicho kinatumbukia kwenye dimbwi kubwa na pana lisiloweza
kukitoa tena.
Akizungumza
na vyanzo vya habari hizi toka jijini Mwanza, alikojichimbia kuhakikisha mchakato wa uchaguzi
wa mameya wa jiji hilo unakwenda vizuri leo, Dk. Slaa alisema dhamira ya kweli
dhidi ya CCM katika kuwaweka vijana kwenye uongozi ili kukinusuru chama hicho
imezimika baada ya Kikwete kuruhusu watuhumiwa wa ufisadi na wakongwe kugombea
uongozi.
“Katika
hili la uteuzi wa CCM, nangojea taratibu zao zikamilike. Tulitegemea CCM muda
huu ni wa kujisafisha, lakini imeshindwa kufanya hivyo. Mimi simung’unyi maneno
kuhusu watuhumiwa wa ufisadi.
Mfano
(anataja) ni fisadi wa fedha za rada. Mimi hapa nilishapeleka ushahidi hadi wa
akaunti namba ya benki yake kwa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini), alisema.
Alisema
inashangaza kuona katika utetezi wa CCM, mtuhumiwa huyo amepatiwa nafasi licha
ya kushindwa kueleza wazi fedha nyingi kwenye akaunti hiyo ya Uswisi alizipataje.
“Mtuhumiwa
mkubwa kama huyu wa ufisadi eti leo CCM inampitisha awe mgombea. Kweli? Sioni
dhamira ya CCM kupambana na vitendo vya kifisadi. Na hata dhamira ya vijana
haipo bali imejitumbukiza kwenye dimbwi ambalo kamwe hakitatoka humo,” alisisitiza.
Kuhusu
Lowassa na tuhuma zake za ufisadi wa kampuni ya kufua umeme wa dharura wa
Richmond zilizosababisha kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008, Dk. Slaa alisema
kiongozi huyo alilazimika kujiuzulu kama sehemu ya kuwajibika, lakini
ameshindwa hadi leo kumtaja mhusika hasa wa kampuni hiyo.
Alisema
kama kweli Lowassa alisingiziwa katika tuhuma hizo, alipaswa kuwaeleza
Watanzania nani anayehusika na ufisadi huo wa Richmond ambayo ilishindwa
kuzalisha umeme licha ya kutumia mamilioni ya fedha za umma.
Kuhusu
wanachama wa CCM ambao majina yao yamekatwa na NEC, Dk. Slaa alisema milango
iko wazi CHADEMA kwa wale wasio mafisadi kujiunga ili kukielekeza chama hicho
kushika dola mwaka 2015.
Alisema
CHADEMA ni chama makini huenda kuliko vyama vingine, hivyo hakiwezi kupokea
wanachama kutoka CCM wanaotuhumiwa kwa ufisadi, vinginevyo kitafunga milango na
mapazia yake.
“Unajua,
kuna watu wanaojulikana kwa ufisadi. Pia wapo wasafi wanaoomba kujiunga na
CHADEMA, hivyo watu safi hawana tatizo kujiunga na CHADEMA kwa ajili ya
kuunganisha nguvu kwenda kuongoza dola mwaka 2015,” alisema Dk. Slaa.
No comments:
Post a Comment