Mwandishi
wa Habari na Mtangazaji wa zamani wa TBC, Jerry Muro ( kushoto) akito salamu
zake kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji cha Bavicha Taifa iliyoketi Mjini
Morogoro kuanzia Septemba 14 hadi 18, mwaka huu.
John Heche , Septemba 17, 2012 alifungua Kikao cha Kamati ya Utendaji ya
Bavicha kilichohudhuriwa na wajumbe kadhaa kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara
na Visiwani.Kikao hicho kilipanga kujadili ajenda mbalimbali za Vijana na
baadaye kufikia kutoa tamko la pampoja kuhusiana na masuala ya kisiasa, kijamii
na kiuchumi.
Hata hivyo katika Kikao hicho , Bavicha kupitia Mwenyekiti wake wa Taifa
, walimkaribisha Mwandishi wa Habari na Mtangazani wa zamani wa TBC, Jerry Muro
ili aweze kuwasalimia wa wajumbe wa Baraza hilo walioanza kukutana tangu
Septamba 14 hadi 18, mwaka huu.Katika salaamu zake , Muro alisema, yenye ni
mwanaharakati na mtu anayependa kusema ukweli, hivyo kwake mtu kama huyo ni
lazima amuunge mkono kama ilivyo kwa vijana wa Bavicha wanavyosimamia kusema
ukweli na kuamua kuwaunga mkono kwa hilo.
No comments:
Post a Comment