To Chat with me click here

Saturday, September 29, 2012

JINSI ILIVYOKUWA KATIKA ZOEZI LA KUMWAGWA JEN. KAMAZIMA



Dk. Edward Hosea ametoa salam za rambi rambi kwa niaba ya Takukuru; Anasema: Marehemu, alihamishiwa TAKURU 1990... Akitokea JWTZ... Hadi anastaafu 2003

Anakumbukwa kwa mengi akiwa taasisi hiyo, na katika uongozi wake, ndipo ilipanuka na kuongeza ofisi hadi wilayani

Atakumbukwa kwa uadilifu na busara Wakati wote wa uongozi wake.


Kwa niaba ya Takukuru, wametoa mchango wa milioni 10


Chuo cha Ulinzi walitoa 1.3m


Mwakilishi wa Chuo cha Diplomasia, Dk.Bernad Achiula, ametoa rambirambi zake Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi na Jumuiya ya Diplomasia, pole kwa familia na kwa mama na watoto na jamaa wote..


Marehem alikua mjumbe wa bodi na makamu mwenyekiti wa bodi 2002-2008


Anakumbukwa kwa mchango wake kuimarisha chuo hasa ktk fani zake za Diplomasia, strategia, na ufumbuzi wa migogoro... Chuoni hapo. Kumbukumbu zipo chuo, Chuo kimetoa laki tano kwa familia


Salam za Tanganyika Law Society, mwakilishi wake metoa  salam. Rugambwa Siriro , mwanasheria amesoma risala kwa niaba ya francis Stola, rais wa Chama cha wanasheria, marehemu alikuwa wakili.

No comments:

Post a Comment