To Chat with me click here

Saturday, September 29, 2012

CCM WASHINDA KITI CHA UMEYA JIJI LA MWANZA.


Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kupitia CCM (katikati) akiwa na Naibu Meya John Minja (CCM) wakitambulishwa na Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe baada ya kutangazwa washindi  kufuatia uchaguzi uliofanyika leo katika ukumbi wa halmashauri ya jiji la Mwanza.

*******************************************

Hatimaye kile kitendawili cha nani atakuwa meya wa jiji la mwanza kati ya vyama viwili vikuu vyenye upinzani mkubwa CCM na CHADEMA kimeteguliwa baada ya chama cha mapinduzi CCM kushinda uchaguzi huo na kutwaa kiti hicho cha umeya wa jiji la mwanza.

Akitangaza matokeo mara baada ya madiwani kupiga kura Mkurugenzi wa jiji la mwanza kabwe amemtangaza Stansilaus Mabula diwani wa kata ya mkolani kuwa meya wa jiji la mwanza baada ya kupata kura 11 na kumwaga chini mpinzani wake kutoka CHADEMA Charless chinchibela aliyepata kura 8.

Nafasi nyingine iliyokuwa ikiwania katika uchaguzi huo ni nafasi ya Naibu Meya wa jiji hilo ambapo Daudi Mkama kutoka CUF kura 8 na John Minja aliyepata kura 10 na kutangazwa rasmi John Minja diwani wa kata ya mbungani kuwa Naibu meya wa jiji lamwanza.

Mara baada ya kutangazwa kuwa meya Mabula ametaka umoja na ushilikiano kutoka kwa madiwani ili kuweza kuwatumikia wananchi kwa nguvu ili kuweza kuwaletea maendeleo na kuliletea sifa jiji la mwanza.

Katibu wa itikadi na uenezi CCM taifa Nape nauye mara baada ya uchaguzi kuisha akajitokeza mbele ya waandishi wa habari kuwapongeza madiwani wa cccm waliochaguliwa kwa nafasi za meya na naibu meya kwa kiuweza kulililudisha jiji la mwanza mikononi mwa ccm.

Amesema kuwa kikubwa ni ushilikiano katika kutenda kazi za wananchi wa jiji la mwanza ili kuweza kuwaletea maendeleo kwa pamoja na kutoa ushilikiano kwa chama cha mapinduzi ili kudumisha umoja na mshikamano.

“Dk. Slaa mara baada ya kuona maji yamemfika shingoni ameamua kutofika katika uchaguzi huu na alikuwa anajua ni jinsi gani uchaguzi utakavyo kuwa na sasa anahamini ya kuwa ccm sio chama cha vurugu kama chama chao na hatuwezi kuongoza kibabe kama wao wananvyozani na tena ninadhani kuwa chadema wameona mavuno ya ubabe wao kuwa hayana umuhimu wowote”. Alisema Nape.

Amesema kuwa ni vyema sasa wanamwanza wakawa na mshikamano na kuacha kufanya maandamano ambayo hayana umuhimu wowote kwao na badala yake wafanye maendeleo na kukaa kwa amani.

 Ni picha ya pamoja Meya Mabula, mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga(katikati) na Naibu meya John Minja wakiwa katika ofisi ya Mstahiki Meya.
Kutoka kushoto ni aliyekuwa Meya wa jiji la Mwanza kabla ya jiji hilo kugawanywa kuwa Manispaa na Halmashauri, diwani Manyarere akiwa na diwani Rose Brown na diwani wa viti maalum ndani ya ukumbi wa Uchaguzi kutafuta Meya na Naibu wake Nyamagana.
 Meya wa jiji la Mwanza (wa3kutoka kushoto) Naibu Meya (wa kwanza kushoto) wakiwa pamoja na Madiwani wa CCM wakimsikiliza mbunge wa viti maalum Maria Hewa (wa pili kutoka kulia) aliyekuwa akisema “Chama kimerudisha heshima yake katika jiji la Mwanza”.

Ikumbukwe kuwa jana kulikuwa na chaguzi mbili za Ma- Meya na Ma- Naibu wake wa Halmashauri ya jiji la Mwanza (Nyamagana) na Manispaa ya Ilemela, baada ya uchaguzi wa Nyamagana kumalizika na wajumbe wake kuondoka ukumbini  ili kuwapisha wajumbe wa wilaya ya Ilemela, nao waliketi katika ukumbi wa uchaguzi wakisubiri kushiriki uchaguzi wa kuteuwa Meya na Naibu Meya wao ambapo uchaguzi huo haukufanyika kufuatia diwani wa kata ya Kitangili kufungua kesi katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kupinga kuvuliwa uanachama, kupinga kuenguliwa katika mchakato wa kuwania nafasi ya Meya hadi hapo uamuzi wa kesi yake utakapo tolewa, kutokana na kuwa na hati ya Mahakama inayomruhusu aidha kuruhusiwa kushiriki kupitia chama chake cha zamani (CHADEMA) au chama chake kutofanya uteuzi wa wagombea.

 Madiwani wa CHADEMA wakiwa na mbunge wao  wa wilaya ya Ilemela Highness Kiwia (katikati) wakisubiri taratibu za uchaguzi ambao hata hivyo haukufanyika.
  Aliyekuwa mgombea nafasi ya Meya wa Manispaa ya Ilemela Abubakar Kapera diwani kata ya Nyamanoro (kulia)   na kushoto kwake ni diwani wa kata ya Kirumba Danny Kahungu aliyekuwa akiwania nafasi ya Naibu Meya Ilemela  wote kutoka CHADEMA ndani ya ukumbi wa uchaguzi kabla ya uchaguzi wao kuahirishwa kutokana na zuio.
Kutoka kushoto ni aliyekuwa Meya wa jiji la Mwanza kabla ya jiji hilo kugawanywa kuwa Manispaa na Halmashauri, diwani Manyarere akiwa na diwani Rose Brown na diwani wa viti maalum ndani ya ukumbi wa Uchaguzi kutafuta Meya na Naibu wake Nyamagana.
 Diwani wa kata ya Kitangili Henry Matata (aliyevuliwa uanachama CHADEMA) akisalimiana na diwani mwenzake Marietha Chenyenge huku mkononi akiwa na hati ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza iliyozuia kufanyika wa Meya na Naibu Meya mpaka pale kesi iliyofunguliwa na diwani huyo kupinga CHADEMA kuteua wagombea wa nafasi hizo, kwa chati  mbunge wa jimbo la Ilemela Highness Kiwia (aliyesimama) akiwa bize na simu yake ya kiganjani, kabla ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa Manispaa ya Ilemela.
 Madiwani wa CCM wilaya ya ilemela kabla ya uchaguzi wao kuahirishwa.

No comments:

Post a Comment