To Chat with me click here

Saturday, September 8, 2012

WAISLAMU WAANDAMANA DAR KULISHINIKIZA JESHI LA POLISI KUWAACHIA WENZAO WALIOTIWA MBARONI KWA KOSA LA KUKATAA KUHESABIWA KATIKA SENSA


Waumini wa Dini ya Kiislamu  wakiwa mbele ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania, Dar es Salaam, walipokwenda baada ya kuandamana Jana mchana wakidai kuachiwa huru kwa waislamu wote waliokamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kukataa kuhesabiwa wakati wa Sensa ya Watu na Makazi.
Askari wa jeshi la polisi wakiwa Barabara ya Azikiwe kulinda doria wakati Waislamu wakiandamana  Makao NMakuu ya Jeshi la Polisi Tanzania, Dar es Salaam Jana.
Baadhi ya wafanyakazi ambao ofisi zao zimo ndani ya Jengo la Exim, wakishuhudia maandamano ya waislamu waliokuwa wamekaa chini mbele ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Dar es Salaam.
Barabara ya Azikiwe ikiwa haina magari mengi kama ilivyozoeleka, baada ya kufungwa kwa muda kuyapisha maandamano ya waislamu.

No comments:

Post a Comment