Waziri wa
mambo ya ndani ya nchi Dkt Emmanuel Nchimbi
Habari
kutoka mkoani Iringa zilizoripotiwa na mwandishi maalum wa mtandao huu kutoka
mjini Iringa zinadai kuwa Kamati iliyoundwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Dkt Emmanuel Nchimbi kwenda kufanya uchunguzi dhidi ya mauwaji ya aliyekuwa
mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoani Iringa na mwenyekiti wa klabu ya
waandishi wa habari mkoani Iringa, Marehemu Daudi Mwangosi imeibiwa katika hoteli
maarufu iliyokuwa imefikia.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Leo ambapo mmoja Kati ya wajumbe wa tume hiyo ameamka na kujikuta mtupu Bila ya Laptop yake yenye nyaraka nyeti za kumwezesha kufanya uchunguzi huo kuibwa.
Inadaiwa kuwa Kamati hiyo pamoja na kuundwa na waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani ya nchi ila bado imekuwa ikifanya kazi katika mazingira hatari zaidi baada ya kuwepo kwa habari kuwa imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu zaidi na makachero wa polisi.
Hata hivyo habari Kutoka ndani ya jeshi la polisi ambazo zinafanyiwa kazi na jeshi la polisi mkoani Iringa zinadai kuwa Kamati hiyo imeondoka asubuhi hii kuelekea Nyololo kuanza kufanya kazi yake .
Habari na Francis Godwin
No comments:
Post a Comment