Polisi
ya Tanzania imewakamata majambazi tisa na kukamata silaha katika operesheni
hiyo katika maeneo ya Pwani na Dar es Salaam.
Polisi
ilikamata silaha saba na risasi 75 kutoka kwa washukiwa, kwa mujibu wa kamanda
wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam Suleiman Kova.
Alisema
kuwa Waburundi wanne, wakiwa na wenzao wenyeji, walikamatwa mjini Dar es Salaam
wakiwa wanamiliki kompyuta tano za mkononi, dola 1,900 (shilingi milioni 3) na
shilingi 70,000 (dola 44) taslimu, pamoja na fedha za Kenya, Rwanda na Burundi.
Kova
alisema kuwa polisi iliwagundua washukiwa hao wa ujambazi baada ya wenyeji
kutoa taarifa kwa polisi.
"Katika
tukio jengine, tuliwatia mbaroni wezi wanne huko Ikwiriri katika eneo la
Pwani," Kova alisema. Walikuwa wamebeba bunduki ya rashasha na risasi 11,
redio za mawasiliano ya njia mbili na vifaa vyengine vya kutiliwa shaka,
alisema.
No comments:
Post a Comment