NI
BAADA YA KUSHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI, ANAKABILIWA NA SHITAKA LA KUFANYA VURUGU
Mwk. wa Chadema Freeman Mbowe |
MAHAKAMA
ya Wilaya Hai, mkoani Kilimanjaro, imetoa hati ya kukamatwa Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, baada ya kushindwa kufika
mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili.
Hati
ya kukamatwa kwa Mbowe, ambaye pia ni Mbunge wa Hai, ilitolewa jana na Hakimu
Mfawidhi wa mahakama hiyo, Denis Mbelembwa, baada ya mbunge huyo kutohudhuria
mahakamani hapo bila taarifa yoyote.
Pamoja na kutolewa hati ya kukamatwa Mbowe, pia hakimu huyo alitoa hati ya kumkamata mdhamini wa Mbowe, Awadh Uronu, kwa kile kilichodaiwa kuwa amekiuka masharti ya udhamini.
Pamoja na kutolewa hati ya kukamatwa Mbowe, pia hakimu huyo alitoa hati ya kumkamata mdhamini wa Mbowe, Awadh Uronu, kwa kile kilichodaiwa kuwa amekiuka masharti ya udhamini.
Hakimu
huyo alitoa hati hiyo, baada ya Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Marwa
Mwita, kuiambia Mahakama kuwa, kitendo cha Mbowe kutohudhuria mahakamani hapo
amekiuka masharti ya dhamana.
Katika shauri hili, Mbowe anakabiliwa na mashitaka ya kufanya vurugu na kumjeruhi Msimamizi wa Uchaguzi, siku ya uchaguzi mkuu mwaka 2010.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Mbowe anadaiwa kufanya vurugu huzo Oktoba 31, katika kituo cha Uchaguzi kiitwacho Lambo.

Inadaiwa
kwamba, mshitakiwa huyo alimshambulia msimamizi huyo, Nasri Othmani na
kumsababishia maumivu makali mwilini.
Mbowe
ameshitakiwa kutokana na kuvunja kifungu namba 240 sura 16 cha Sheria ya Makosa
ya Jinai.
No comments:
Post a Comment