VURUGU
KUBWA ZAIBUKA, MKUTANO WAVUNJIKA, MBUNGE KIWIA AJIFICHA CHINI YA
MEZA KUJINUSURU
KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Ilemela jana kilivunjika, baada ya
kutokea vurugu kubwa, zilizosababisha wajumbe kutwangana makonde.
Kikao hicho kilikuwa kikifanyika katika Hoteli ya Ladson iliyopo Bwiru, kwa ajili ya kupitisha majina ya wagombea wa nafasi ya meya na naibu meya wa Manispaa ya Ilemela,
Hata hivyo askari polisi walifanikiwa kuwasili mapema hotelini hapo na kuwatawanya wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na vijana wa chama hicho, waliokuwa wamevamia kikao hicho.
Vurugu hizo zilizodumu kwa saa moja na kusababisha kizaazaa hicho, zilizuka baada ya uongozi wa Kamati ya Utendaji wa chama hicho Wilaya ya Ilemela, kukaidi amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.
Mahakama hiyo ilikuwa imezuia kufukuzwa uanachama wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kitangiri, Henry Matata, hadi pale kesi ya msingi itakapomalizika.
Mahakama hiyo pia iliamuru diwani huyo aendelee kuwania nafasi ya umeya wa Ilemela, ambapo kamati hiyo ilizuia jina la Matata lisiwemo katika majina ya watu wanaogombea nafasi ya umeya.
Dalili za kuvurugika kwa hali ya amani ilionekana tangu mapema, baada ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ilemela (OCD), Debora Magiligimba, kuwasili katika hoteli hiyo akiwa katika gari lililokuwa limebeba askari polisi.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Yunusu Chilongozi, alisema kikao hicho
hakitambui amri hiyo ya mahakama, hivyo hakukuwa na haja ya kumruhusu Matata
kuwa miongoni mwa wagombea.Kikao hicho kilikuwa kikifanyika katika Hoteli ya Ladson iliyopo Bwiru, kwa ajili ya kupitisha majina ya wagombea wa nafasi ya meya na naibu meya wa Manispaa ya Ilemela,
Hata hivyo askari polisi walifanikiwa kuwasili mapema hotelini hapo na kuwatawanya wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na vijana wa chama hicho, waliokuwa wamevamia kikao hicho.
Vurugu hizo zilizodumu kwa saa moja na kusababisha kizaazaa hicho, zilizuka baada ya uongozi wa Kamati ya Utendaji wa chama hicho Wilaya ya Ilemela, kukaidi amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.
Mahakama hiyo ilikuwa imezuia kufukuzwa uanachama wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kitangiri, Henry Matata, hadi pale kesi ya msingi itakapomalizika.
Mahakama hiyo pia iliamuru diwani huyo aendelee kuwania nafasi ya umeya wa Ilemela, ambapo kamati hiyo ilizuia jina la Matata lisiwemo katika majina ya watu wanaogombea nafasi ya umeya.
Dalili za kuvurugika kwa hali ya amani ilionekana tangu mapema, baada ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ilemela (OCD), Debora Magiligimba, kuwasili katika hoteli hiyo akiwa katika gari lililokuwa limebeba askari polisi.
Pamoja na juhudi za polisi kuwataka viongozi hao kuheshimu amri ya mahakama, viongozi hao walizidi kukaidi, ndipo OCD na askari wake walipoamua kuondoka katika eneo hilo na kuwaacha wanachama pamoja na viongozi wakiendelea kuvutana.
Muda mfupi baada ya askari kuondoka, kundi kubwa la vijana wa Chadema lilivamia katika ukumbi huo na kuanza kutembeza kichapo kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji, hali iliyosababisha vurugu kubwa.
Makundi hayo ya vijana ni miongoni mwa wafuasi wa chama hicho wanaopinga kitendo cha diwani huyo na mwenzake wa Kata ya Igoma kuvuliwa uanachama.
Katika vurugu hizo, Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia (Chadema), aliyekuwa miongoni mwa wajumbe hao, aliamua kujificha chini ya meza kama njia ya kujinusuru.
Wakati Kiwia akiingia uvunguni mwa meza kujinusuru, baadhi ya wajumbe walikimbia huku na kule na wengine waliamua kujificha chooni, ili kujinusuru.
Kutokana na vurugu hizo, uongozi wa hoteli hiyo uliamua kupiga simu polisi ambapo kikosi cha polisi wenye silaha na zana nyingine walifika na kuwatawanya vijana hao.
Akizungumza na Mtanzania baada ya vurugu hiyo, Chilongozi alizidi kusisitiza msimamo wa kamati yake kwamba, hapakuwa na sababu za kuahirisha kikao hicho.
Chilongozi alifafanua zaidi na kusema kuwa kamati yake iliamua kumzuia Matata kutokana na maelekezo yaliyotolewa na viongozi wa juu kutoka makao makuu ya chama.
Akizungumza na waandishi wa habari Matata alisema kuwa, kamati hiyo imeonyesha dharau kubwa kwa mahakama na kusema kuwa, wajumbe hao wanapaswa kuchukuliwa hatua ili iwe fundisho.
“Amri ya mahakama haiwezi kuvunjwa na wahuni wachache kwa manufaa yao, nitapigania haki yangu hadi pale kitakapoeleweka, siwezi kukaa kimya,” alisema Matata.
Mtazania
No comments:
Post a Comment