To Chat with me click here

Wednesday, September 26, 2012

MTOTO JULIANA MWINUKA AANZA MATIBABU, MCHANGO WAKO MDAU BADO UNAHITAJIKA ZAIDI


Mtoto Juliana Mwinuka akiwa amelazwa Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam kwa matibabu ,huku  pembeni mdau  wa mtandao  huu Jemida Kulanga  kutoka  mkoani Iringa akimpa pole ,Jemida amekuwa msaada mkubwa  kufanikisha mtoto  huyo kuonwa na  watanzania baada ya  kufika  kijijini na kuleta taarifa  hizi katika mtandao  na leo wadau  kuchangia hadi  kufika hapa mtoto Juliana.

Mtoto Juliana Mwinuka mkazi wa kijiji Cha Mavanga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe amelazwa katika Hospitali ya CCBRT wodi la wagonjwa wa Macho tunaendelea kuwashukuru wote wanaoendelea kutoa michango yao kunusuru uhai wa mtoto Juliana ambaye ni yatima.

Mtandao huu unaendelea kuwapongeza wote wanaoendelea kuguswa na kuungana na wadau wengine kumchangia fedha za matibabu ,mtoto Juliana kama anavyoonekana akiwa ameunga uso wake kwa moto ni yatima anahitaji msaada wako ili kunusuru maisha yake waweza kutuma mchango wako kwa njia ya M-PESA katika namba hii 0754 026 299 au Tigo Pesa 0712 750199 namba hizi za Bw Francis Godwin wa mtandao wa Francis Godwin Blog.

Nawaomba tuungane kufanikisha kuokoa maisha ya mtoto Juliana Mwinuka na Mungu atatuongezea zaidi.

No comments:

Post a Comment