Mhe. Freeman A. Mbowe |
Leo ni siku ambayo Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe, ametimiza miaka 51 tangu kuzaliwa kwakwe, vilevile anatimiza miaka 21 ya kuongoza Upinzani katika mapambano ya ukombozi wa Taifa letu toka katika makucha ya mafisadi wachache ambao wamekuwa wakilifilisi Taifa kwa kijilimbikizia mali na kuwaacha watanzania wakiwa maskini siku hadi siku.
Katika harakati zake hizi za kisiasa katika kutetea wanyonge na kulihakikishia Taifa hili ukombozi kamali na wa kweli, Mhe. Mbowe amekuwa akikumbana na changamoto mbalimbali kama vile, kushtakiwa, kusingiziwa mambo mbalimbali kwa chama chake n.k
Lakini katika haya yote ameendelea kuonesha msimamo dhabiti wa kutetea na kusimamia kile ambacho yeye binafsi na Chama chake kwa pamoja wamekuwa wakiamini. Hii imeonesha dhamira ya dhati ya Mhe. Mbowe katika kuleta mageuzi ya kisiasa nchini ili kutoa fursa sawa ya kimaendeleo kwa kila mtanzania tofauti na ilivyo sasa.
Katika siku yake hii ya kuzaliwa, Mhe. Mbowe ameandika haya katika ukurasa wake wa FACEBOOK (FB);
No comments:
Post a Comment