To Chat with me click here

Monday, September 24, 2012

MSAMARIA MWEMA MDAU WA MTANDAO HUU AJITOLEA KUMSAFIRISHA MTOTO JULIANA KWENDA DAR KUANZA MATIBABU

Mtoto Juliana Mwinuka.
Msamaria  mwema mdau wa mtandao huu   kutoka jijini Dar es Salaam ameungana na  wadau  wa mtandao (Blog)  wa Francis Godwin kujitolea gharama zote za usafiri kutoka kijiji cha Mavanga Ludewa hadi jijini Dar es Salaam ili kumwezesha mtoto  Juliana Mwinuka mkazi wa Mavanga wilaya ya Ludewa  ambaye amekuwa akitabika nyumbani na majeraha ya  moto kufika Hospitali  kuanza matibabu  wakati jitihada za mtandao  huu kuendelea kumchangishia  fedha zinafanyika.

Mdau huyo ametoa  kiasi cha shilingi 162,000 kama nauli ya  bibi wa mtoto  huyo ,mgonjwa mwenyewe na msindikizaji mmoja  kutoka Ludewa hadi Dar es Salaam .

Kutokana na jitihada  hizo tayari  uongozi  wa mtandao  huo  umefanya mikakati ya  kufikisha  fedha  hizo na  kumpata kijana Geophrey Katambala wa  shirika la Miso ambaye amepatikana kwa msaada wa mwanarahakati Jemida  Kulanga ambaye ndie alioweza  kufikisha taarifa ya tatizo la mtoto  huyo katika mtandao  huo .

Hivyo  basi mgonjwa  huyo leo anatarajia  kufika jijini Dar es Salaam Tanzania kwa ajili ya kuanzishiwa matibabu ,wewe kama mdau na msamaria  mwema unaombwa  kuungana na wadau  wengine  kunusuru maisha ya mtoto  Juliana na pia mtandao  huu unawapongeza  wote ambao  wamenyosha mikono yao na kuchangia kulingana na uwezo  wao na Mungu awazidishie daima.

Hawa hapa chini ndio ambao wameanza kuguswa na tatizo la mtoto huyo kwa kuchangia fedha kwa njia ya M-PESA kwa namba 0754 026299 ama Tigo Pesa 0712 750199

Hashimu Mbambo (Tsh. 5,000), Neema Ayoub (Tsh 15,000),Onesmo Lulandala(Tsh 10,000),Gasto Mgeni (Tsh. 20,000)na Allin Allin (Tsh 10,000) na Mussa Ayoub (Tsh 10,000)mmiliki wa mtandao huo wa Francis Godwin kwa niaba ya watanzania wote anapenda kuwapongeza wote walioguswa na tatizo la mtoto Julian Mwinuka na kuwaomba wengine zaidi kujitokeza kuchangia chochote kwa namba hizo hapo juu.

NAWAOMBA TUENDELEE KUCHANGIA FEDHA KWA AJILI YA MTOTO JULIANA MWINUKA UHAI WAKE UPO MIKONONI MWETU WASAMARIA WEMA

MAXMILLIAN KATTIKIRO BLOG INAUNGANA NA WADAU WENGINE WOTE KATIKA KUUNGA MKONO JUHUDI HIZI ZA KUMSAIDIA MTOTO JULIANA ILI AWEZE KUPATA MATIBABU NA KUPONA HARAKA. 

MWENYEZI MUNGU AWAZIDISHIE KWA UKARIMU WENU KWANI KUTOA NI MOYO NA SI UTAJIRI!.

No comments:

Post a Comment