Benson
Singo Masalamakali Kigaila,mkuu wa oparesheni ya M4C akiongea na waandishi leo
Iringa
Ikiwa ni
siku tano zimepita toka kuuwawa kwa mwandishi wa habari wa channel ten na
mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Iringa Daudi mwangosi katika vurugu
baina ya polisi na CHADEMA huko nyororo mafinga.
Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo kupitia viongozi wake Iringa wameongea na
waandishi wa habari kuhusu kile kilichotokea.
Akiongea
na waandishi wa habari Iringa leo Mkurugenzi wa mafunzo na operesheni ya
Movement For Change Taifa Benson kigaila, ameeleza kuwa lengo kubwa la Chadema
tarehe 2.09.2012 kule Nyororo walikuwa na lengo la kufungua matawi na kufanya
vikao vya ndani na wanachama wao na sio kufanya mikutano ya hadhara kama
inavyosemekana.
Aliendelea
kuleleza kuwa wakiwa katika ufunguzi wa tawi katika ofis ya kata Nyororo Polisi
wafika na kutangaza kuwa watawanyike na wakamueleza RCO kuwa wapo kwaajili ya
kufungua tawi na kufanya kikao cha ndani na kwamba polisi wakiingilia ndio
watakao kuwa wanachochea vurugu.
Aidha
Kigaila ameongeza kuwa wakati huo huo wakifungua Tawi hilo vyama vingine kama
CCM nchi nzima walikuwa wakifanya chaguzi katika ngazi za Wilaya lakini
hawakuzuiwa kwa kile kinasemwa kuwa ni kuingilia zoezi la sensa.
Baada ya
kufanikiwa kufungua tawi walitangaza kuwa wanaelekea ofisi ya kata ili
wakafungue tawi lingine lakini alipoingia RPC Kamuhanda ndipo alipoagiza na
kusema kuwa hakuna kuzindua tawi ni kutawanisha watu na kufunga mkutano”
alisema Kigaila.
Wakati
wakielekea katika ofisi ya kata Marehemu mwangosi alimueleza kigaila kuwa
anawasiwasi alipokuwa akirekodi wengi wa polisi wanaonekana si wa Iringa jambo
ambalo anaeleza kuwa ndicho chanzo kikuu cha kuuwawa kwake. Huku akihoji kuhusu
kamera na laptop za marehemu kutoonekana na kutotolewa taarifa mpaka sasa.
Naye katibu
mkuu wa Zanzibar Hamadi Yusufu akielezea maneno ya mwisho ya marehemu alisema
kuwa marehemu alikuwa akilalamika kuwa wamwachie kwani yeye yuko kazini
wasimuue kwani anatekeleza majukumu yake “ Jambo ambalo polisi hao
hawakuliktilia maanani nakuendelea kumpiga mpaka umauti ulipomfika.
Aidha
Hamadi ameeleza kuwa wao kama viongozi walikuwa katika tukio hilo wako tayari
kutoa ushaidi mbele ya tume huru itakayoundwa na si Tume iliyoundwa na Jeshi la
polisi au Waziri Nchimbi kwasababu kwa macho yao waliona polisi ambao
wanasimamiwa na wizara yake wakitekeleza dhana hiyo.
Katibu
wa Baraza la Vijana Chadema(BAVICHA) Deogratias Munishi ameeleza “kuhusu kauli
ya Msajili ya Vyama John Tendwa kuwa haina maana kwani alitegemea yeye kama
mlezi wa vyama vya siasa angefika katika eneo la tukio ili aweze kuwa na
ajionee hali halisi vyama anavyovilea yeye vikinyimwa fursa ya kufanya kazi zao
kama vyama vya siasa”
No comments:
Post a Comment