VIJANA
WAKE WASEMA SASA YATOSHA
BARAZA
la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) leo linatarajiwa
kuanika hadharani ukweli wa mauaji ya raia yanayodaiwa kufanywa na vyombo vya
serikali katika mikoa kadhaa hapa nchini.
Kamati
ya Utendaji ya BAVICHA, inayokutana mjini Morogoro, imesema itaweka wazi
sintofahamu ya mauaji hayo yenye mwelekeo wa kisiasa bila uchunguzi huru
kufanyika ili hatua stahili zichukuliwe kwa wahusika.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, BAVICHA imesema kuwa wamelazimika
kufanya hivyo kwa kuwa inaamini haki ya kuishi hata kama ni ya raia mmoja, ina
thamani kubwa kuliko kitu kingine chochote.
Bazara
hilo limesema kuwa mauaji ya kada wao Mbwana Masudi, ambaye alitekwa na kuteswa
mara baada ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunda alikutwa ameuawa kikatili na
watu ambao wanaaminika kuwa wafuasi wa CCM.
Wamesema
hata baada ya uchaguzi wa Arumeru, kulikuwa na matukio mawili ya mauaji ambayo
yote kwa namna moja yamehusishwa na siasa. Tukio la kwanza ni lile ambalo
vijana watano walikutwa wameuawa huko Chekeleni, Arumeru, wakati tukio la pili
ni lile lililomhusisha kiongozi wa CHADEMA, kata ya Arumeru, Msafiri Mbwambo,
ambaye aliuawa kwa kuchinjwa.
“Mauaji
ya namna hiyohiyo yamefanyikwa hivi karibuni katika mkoa wa Morogoro ambako
kijana mmoja, Ali Zona, aliuawa na polisi wakati jeshi hilo lilipovuruga
mapokezi ya viongozi wa CHADEMA kwenda kwenye mkutano mkubwa wa hadhara.
Wamesema
hali hiyohiyo imejirudia karibuni kabisa katika kijiji cha Nyololo, Iringa,
ambapo mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daud Mwangosi, aliuawa kikatili na
kinyama na Jeshi la Polisi kwa kulipuliwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.
“Kwa
namna yoyote ile Kamati ya Utendaji ya BAVICHA haiwezi kufumbia macho mauaji
haya ambayo kwa kweli yana nia ya kudhibiti kasi ya mabadiliko ambayo watawala
wanaiona kuwa inazidi kupamba moto.
Katika
mauaji haya, hakuna hatua zozote za makusudi zilizochuliwa dhidi ya wale
waliohusika na kikubwa serikali kupitia vyombo vyake imekuwa ikifanya mzaha
katika kushughulikia jambo hili. Mauaji haya yanayotekelezwa na jeshi la polisi
kwa amri za serikali ya CCM yamekuwa na dhamira moja tu ya kutaka kuupotosha
umma kuwa CHADEMA ni chama cha fujo,” wamesema.
Waituhumu CCM kufadhili vijana wake
Katika
hatua nyingine BAVICHA imekishukia Chama cha Mapinduzi kwa madai ya kufadhili
vijana wake na kuwaweka kwenye makambi ambako wanafundishwa mbinu haramu za
kudhuru raia wenzao ambao wanaonekana kuipinga hadharani.
Vijana
hao wamesema wanao ushahidi wa kutosha unaodhihirisha kuwa mafunzo hayo
yanatolewa na baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi, kama
ilivyofanywa kwenye makambi maeneo ya Irmaba, Singida, na Tabora wakati wa
uchaguzi mdogo wa Igunga.
Aidha
CCM imeendelea kutumia vijana kwa kuwakodi kutoka sehemu mbalimbali na
kuwapeleka sehemu nyingine ya nchi kwa lengo la kutibua na kufanya fujo kwenye
mikutano ya CHADEMA. Hali hii inathibitishwa na tukio la Ndago, mkoani Singida.
Askofu Mkuu Mtega avunja ukimya
Huko
mjini Songea, mwandishi wetu Julius Konala, anaripoti kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo
Kuu Katoliki la Songea Mhashamu Norbert Mtega amevitaka vyombo vya dola kuacha
mchezo wa kutumia silaha kali hovyohovyo na kuchochea machafuko yanayowaumiza
watu wasio na hatia.
Mhashamu
Mtega alitoa kauli hiyo jana wakati wa sherehe za shirika la Mabinti wa Maria
Imaculete DMI, na kuonya kuwa machafuko yanayozikumba nchi nyingi duniani,
yalianza kwa mtindo unaoonekana kwa sasa hapa nchini.
Askofu
Mtega bila kutaja tukio lolote, alisema madhara yanayoanza kuonekana nchini
yamewagusa zaidi kina mama na watoto ambao hawana uwezo wa kujitetea na
kuwafanya waangamie bila sababu za msingi.
“Nawaambieni
kama tutaachilia mambo haya ya kutumia silaha hovyohovyo yakaendelea kwa kweli
tutakuwa tunatafuta machafuko ambayo yatawaumiza watu wasiyo na hatia kabisa,”
alisema.
Kauli
ya Askofu Mtega inakuja siku chache baada ya kutokea kwa mauaji ya kikatili ya
mwandishi wa habari wa kituo cha Runinga cha Channel Ten, Daud Mwangosi, mkoani
Iringa, baada ya kupigwa bomu na askari polisi.
Mauaji
ya Mwangosi ambayo yalitikisa nchi, yalitokea baada ya askari polisi kuvamia
shughuli za ufunguzi wa ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
katika kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa.
Hivi sasa, tume na kamati
kadhaa zimeundwa kuchunguza sababu za mauaji hayo, ambapo jeshi la polisi
limemfikisha mahakamani askari anayedaiwa kumuua mwandishi huyo wa habari.
No comments:
Post a Comment