NI
KENYA MACHI 2013, UGANDA 2016 NA TANZANIA OKTOBA 2015. VYAMA VYA UPINZANI
VITAFANIKIWA! MUHURA WA WANAWAKE KUWA MARAIS
MARAIS watatu katika nchi za Afrika Mashariki watapatikana katika uchaguzi mkuu ujao, unaotarajiwa kuanza kufanyika tangu mwezi wa machi mwakani. Kenya itafanya uchaguzi mkuu Machi 2013, Tanzania Oktoba 2015 na baadaye Uganda. Chaguzi hizi zina umuhimu mkubwa katika Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika. Marais wapya wanaweza kuja na fikra mpya kwa nchi zao na kwa jumuiya kwa ujumla.
Shauku ya watu wengi ndani na nje ya Afrika Masharika ni kwa vipi vyama vya upinzani vinaweza kuingia madarakani kidemokrasia na pia uwezekano wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa na marais wanawake kutokana na upepo unavyoelekea.
kuanzia sasa katika kipindi kisichopungua miezi sita ijayo na kuendelea. Kenya uchaguzi utakuwa Machi 2013, Uganda ni 2016 na Tanzania 2015. Uchaguzi huu una umuhimu mkubwa katika Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Uchaguzi ujao wa nchi za Afrika Mashariki una mengi ya kuangalia , kujifunza na kuona jinsi gani demokrasia inavyo imarika na kupanuka. Tanzania itakuwa inafanya uchaguzi mkuu kwa mara ya tatu katika mfumo wa vyama vingi, huku Cha Cha Mapinduzi CCM kikiendelea kuwa chama tawala, Kenya inaingia katika uchaguzi mkuu baada ya kuiondoa Kenya African National Union- KANU, kilicholeta Uhuru wa Kenya. Utawala wa Uganda uliingia madarakani baada ya vita vya mistuni chini ya kikundi cha National Resistance Army (NRA ) kilichoongozwa na Rais Yoweri Museveni, baadaye alikibadilisha kikundi cha mapambano hicho na kuwa chama cha kisiasa.
Wakati muda wa uchaguzi mkuu unapokaribia wagombea urais kupitia vyama vyao vya siasa tayari hekaheka zimepamba moto kufanya kampeni za kuwanadi wagombea . Nchini Kenya ambako uchagguzi wake unafanyika machi, 2013 harakati za kunadi wagombea zimefikia hatua ya kuashiria mapambano makali zaidi kwa wagombea maarufu katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.
Ni wazi kwamba kutokana na mfumo wanasiasa wengi ndivyo wanavyatangaza kutaka kugombea urais. Hata hivyo kutoka kwa wananchi wenyewe, akina mama ambao wamejijengea sifa kwa kuchapa kazi za kitaaluma na uongozi wa kisiasa wameanza kutajwa.
Dunia ya wanaume itapambana na wanawake wenye uwezo ,upeo na uwezo wa kuongoza. Ametajwa Mama Janet Museveni Waziri wa Maendeleo ya Karamoja huko Uganda. Ametajwa Mama Martha Karua, Mbunge, mwanasheria na Waziri wa zamani wa sheria na Katiba katika Serikali ya Kenya. Yupo Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, Mbunge ,Waziri wa Arthi, Makazi na Mipango Miji katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia aliwahi kuwa Mkurungezi Mkuu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi, ( UN-Habitat ) ,Nairobi, nchini Kenya.
Nchini Uganda bado hali halisi haijaonyesha mwelekeo wa kuanza harakati mapema kwa wagombea wake kujitokeza kama ilivyo katika nchi za Tanzania na Kenya, ambako watu wenye nia ya kuwania urasi wameanza kusikika mapema. Hata hivyo kuna tetezi za chini kwa chini kuwa mama Janet Museveni na Jenerali Mstaafu, Gregory Mugisha Muntuyera, anayefahamika kwa jina Mugisha Muntu ndio wanaotajwa kumrithi Yoweri Museveni.
Wachambuzi wa masuala ya siasa, wanatafsili mchuano mkali utakuwa kati ya wagombea wawili nchini Kenya , Raila Odinga anayepigiwa upato kuwa mrithi wa Mwai Kibaki na mama machachariMartha Karua, aliyepachikwa sifa ya Iron Lady, kuwa ni mgombea anaonyesha uwezo wa kumkaba koo Raila Odinga.
Nchini Tanzania mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu ndani ya Chama (CCM).Tayari chaguzi ndogo zimeanzia ngazi ya shina, tawi, kata na nzima nzima. Sasa mchakato unaendelea katika ngazi ya Wilaya na Mkoa, kabla ya Mkutano Mkuu wa Taifa Oktoba mwaka huu. Kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi mara nyingi hutoa mgombea ambaye ndiye hutarajiwa kushinda katika uchaguzi mkuu, ni tafsiri isiyo na shaka kuwa, chama hicho kimeanza kuweka ajenda ya kupata ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.
Mkutano mkuu huo, unatarajiwa kubeba ajenda kuu, ya namna bora ya kumpata mgombea sahihi, makini, mwaadilifu mwenye kaliba kubwa anayeuzika kwa wananchi. Ilihali ikijulikana nchi inakabiliwa na changamoto ya kiuchumi, japokuwa changamoto hizo zimekuwa zikitafutiwa ufumbuzi.
Hali ya kudororo kwa uchumi siyo ya Tanzania pekee japo siyo sababu tosha kwa serikali iliyoko madarakani kukwepa wajibu na majukumu yake ya kuinua hali ya uchumi endelevu kwa manufaa ya maendeleo ya wananchi. Nchi nyingi duniani zinateswa na suala la kuporomoka kwa uchumi na ukosefu wa ajira. Nchi za Marekani, Ulaya na nyingi za Afrika hazijasalimika.
Uchambuzi na maoni mbalimbali inaelekea kuwa Waziri wa Ardhi na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na aliyekuwa Waziri Mkuu aliyejiuzuru Edward Lowasa, ni miongoni mwana CCM mmoja wanaoweza kuteuliwa kuwa mgombea urais.
Maoni na uchambuzi unawapa nafasi viongozi hao wawili kutokana na uchapakakazi wao. ProfesaTibaijuka ana uzoefu wa mikakati na mbinu katika nyanja za uongozi, na Lowasa katika vipind i taofauti alionyesha utumishi wake kwa umma, katika kutoa uamuzi mgumu katika masuala mazito.
Kupitia uchambuzi, maoni na tathimini iliyopatikana kupitia mahojiano na wataalam wa masuala ya siasa inawezekana kuwa na marais watatu wapya wa nchi za Afrika Mashariki, kupitia ama vyama tawala na pia uwezekano wa kupata marais hao kutoka vyama vya upinzani.
Suala la uchumi ni ajenda inayotarajia kuwakaba koo wagombea urais Afrika Mashariki, suala la kuporomoka kwa uchumi, wananchi wake wanateswa na hali ya maisha kuendelea kuwa magumu kila kukicha, wananchi wa nchi hizi wanataka nchi zao kuinua uchumi, ili wapate unafuu wa maisha.
Rwanda na Burundi nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hazitakuwa na uchaguzi mkuu. Lakini kwa kiasi chake zinaonyesha mafanikio , licha ya kupitia kipindi kigumu cha migogoro na vita kunaashiria neema kwa wananchi wake, hususan Rwanda, inayoelezewa kuwa nchi hiyo imefanikiwa kwa kiasi na kiwango cha kuridhisha kuinua uchumi wake na kupigiwa mfano.
Vuguvugu na joto la uchaguzi wa Kenya, linavuta hisia na changamoto kubwa ndani na nje ya Kenya. Historia za wanaowania kiti cha urais, wana mivuto yao katika jamii ya Wakenya, ambao ni Martha Karua na Raila Odinga. Moto wa Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta na William Ruto unapunguzwa na kesi inayowakabili katika Mahakama ya ICC- The Hague. Ilhali Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka na Naibu Waziri Mkuu Musalia Mudavadi ,ni wagombea wanaopewa nafasi finyu kumpiku Raila Odinga, kutokana na kampeni zake kuwateka wananchi wa kada ya chini na kati ambao ndio wengi.
Raila anayeongoza chama cha upinzani katika Serikali ya umoja wa kitaifa na anaendelea kubadili hali ya siasa , mtazamo na tathimini ya siasa za Kenya, ambazo hutawaliwa na ukabila , doa ambalo anajitahidi kuliondoa , kwa mujibu wa maoni ya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini Kenya.
Katika tathimini na maoni mbalimbali yaliyopatikana inaelezwa kuwa chaguzi za marais katika Afrika Mashariki , kuna uwezekano wa kuwepo na rais mwanamke katika nchi za Afrika Mashariki. Wakigombea Martha Karua nchini Kenya, Uganda Janet Museveni na Tanzania Profesa Anna Tibaijuka.
Aidha, vyama vya upinzani katika chaguzi zijazo vinapewa nafasi kubwa kushinda, uwezekano huo unaonekana zaidi nchini Kenya ,ambako Raila Odinga ,anapewa nafasi kubwa ya kushinda. Ilhali nchini Uganda kuna Jenerali mstaafu , Mugisha Muntu, aliyewahi kuwa Kamanda ngazi ya juu katika Jeshi la Ulinzi la Uganda( UPDF), ni mshindani mkubwa iwapo atafanikiwa kuteuliwa kugombea na kushindanishwa na Janet Museveni.
Upinzani nchini Tanzania inaelezwa na wachambuzi wa masuala ya siasa, kuwa vyama vya upinzani bado vinasuasua ,kuonyesha dira, mikakati, mbinu na dhima ya dhati inayoweza kushawishi umma kuwa na imani ya kushika dola na kuwa mbadala wa CCM.
No comments:
Post a Comment