VIJANA
MWANZA WAIMBA ‘PEOPLE’S POWER, HATUITAKI CCM’
WAZIRI
Mkuu Mizengo Pinda, jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kushindwa
kuhutubia maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza kwa muda
kutokana na wananchi wengi kumzomea.
Kiongozi
huyo alikumbana na kisanga hicho cha aina yake akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Mwanza, Clement Mabina pamoja na Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Evarist Welle
Ndikilo.
Pinda
na viongozi hao, walikumbana na zomeazomea hiyo kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika viwanja vya Sahara jijini hapa, ikiwa ni hitimisho la ziara ya
Waziri Mkuu huyo ya siku saba mkoani Mwanza.
Chanzo
cha Pinda na viongozi hao kuzomewa mkutanoni hapo, ilitokana na kile
kilichoonekana kuwepo kwa kero nyingi zilizodaiwa kushindwa kupatiwa ufumbuzi
na Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete.
Kitendo
hicho cha wananchi kilimlazimisha Pinda kushindwa kuhutubia kwa muda, huku
akionekana kujawa jazba.
Sababu
nyingine ya wananchi kuzomea, ni hatua ya Pinda kuwaambia wananchi hao watoke
mjini waende vijijini wakalime waachane na mambo ya upinzani wa kisiasa.
Pinda
alitoa kauli hiyo baada ya kundi la vijana mkutanoni hapo kuonesha alama ya V,
bendera ya CHADEMA na nyimbo za Peoples, Power.
Baada
ya kuzidi zomeazomea hiyo, Waziri Mkuu, Pinda alilazimika kumuita mbunge wa
Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), aliyekuwa meza kuu, kisha kusema:
"Nyamazeni basi!. Wenje...hii ndiyo serikali ya siku chache zijazo. Kwa
namna hii naona hamuwezi, maana itakuwa ni vurugu asubuhi hadi jioni".
Akazomewa kisha wakaimba hatutaki CCM, hatutaki CCM. .
Baada
ya kuona hivyo, Pinda akacheka na kusema: "Hahahaaaaa, hata mkiimba
peoples power, CCM ndiyo inayowaongoza". Akazomewa tena kisha Pinda
akashindwa kuendelea kuzungumza jukwaani.
Akahutubia
mkutanoni hapo, Pinda aliwataka wananchi hao waache ushabiki wa kisiasa, na
kwamba halmashauri ya jiji la Mwanza inayoongozwa na CHADEMA, ndiyo itapaswa
kulaumiwa kama itashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wake.
"Hapa
jiji la Mwanza linaongozwa na CHADEMA. Meya wa CHADEMA, mwenyekiti wa Mipango
miji wa CHADEMA, Naibu Meya ni wa CHADEMA. Lakini kama wameshindwa kuweka
mipango mikakati ya kuwasaidia tutasema hawafai," alisema kisha akazomewa
kwa mara nyingine.
Baada
ya zomeazomea hiyo kuonekana kumwelemea Waziri Mkuu huyo, Mkuu wa mkoa wa
Mwanza, Ndikilo alilazimika kuingilia kati kwa kusema: "Wanaozomea
tunawafahamu, na tunawafahamu waliowaleta hapa ili mje kufanya nini".
Akazomewa.
Hata
hivyo, baada ya hali kutulia kidogo, Pinda aliendelea kuhutubia huku akiwataka
wananchi wa jiji la Mwanza waondoke mjini waende vijijini wakalime, jambo
lililoonekana pia kuwakasirisha wananchi wengi kisha kumzomea tena.
Ingawa
Pinda alilazimika kutumia muda mfupi kutoa hotuba yake, aliwaomba wana Mwanza
washirikiane kuleta maendeleo yao, na kwamba iwapo tatizo ni Mkurugenzi wa jiji
suala hilo litaangaliwa.
Aliwaomba
wadumishe amani iliyopo hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na
Serikali kupambana na vitendo vya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria, ili kuweza
kuzua samaki wadogo wasivuliwe kisha kuharibu mazalia ya rasilimali hiyo.
"Jambo
jingine ninalotaka kuwaeleza hapa leo ni hili la uvuvi haramu. Samaki ndani ya
Ziwa Victoria wameisha...na hii ni kwa sababu ya uvuvi usiozingatia sheria.
Tushirikianeni kupambana na vitendo hivi", alisema Pinda kisha akazomewa
tepa.
No comments:
Post a Comment