Diwani wa kata ya
Gongo la Mboto Mh. Silaa akimkabidhi Bi. Hadija ambae ni mkazi wa mtaa wa
Kilimo; ndoo ya maji aliyoyachota kutoka katika kisima alichokikabidhi kwa
wakazi wa mtaa huo hapo Jana.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni
diwani wa kata ya Gongo la Mboto akizindua rasmi kisima cha maji kilichojengwa
kwa ushirikiano wake na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kilimo Bw. Moshi
Mwaluko
Baadhi ya wakazi wa
kata ya Gongo la Mboto wakimsikiliza kwa makini Diwani wa kata yao Mh. Jerry
Silaa (hayupo pichani), wakati akiwakabidhi vifaa vya michezo pamoja na kisima
cha maji hapo jana
Mh. Jerry Silaa
akichota maji kwenye kisima alichokikabidhi kwa wakazi wa mtaa wa Kilimo, kata
ya Gongo la Mboto kama ishara ya kufunguliwa kwake rasmi , huku baadhi ya
viongozi na wakazi wa mtaa huo wakishuhudia
Mh. Jerry Silaa akimkabidhi seti ya vifaa vya
michezo, mmoja kati ya manahodha wa timu zilizoshiriki ligi ya mpira wa miguu
katika kata ya Gongo la Mboto ijulikanayo kama Jerry Cup
No comments:
Post a Comment