Pichani ni Vipeperushi
vilivyotolewa na Waumini wa Dini ya Kiislamu kabla ya maandamano leo.
Wakati Zanzibar Sakata la Waislamu kuendeleza
kitimtim kufuatia kutoonekana kwa Kiongozi wa Kundi la Uamsho Vurugu
zimeendelea kutawala eneo la Darajani na kusababisha Polisi kulazimika kutumia
mabomu ya machozi kutawanya watu.
Jijini Dar es Salaam hali si tofauti na hiyo
maeneo ya Kariakoo maduka kadhaa yamefungwa kufuatia vurugu kama hizo baada ya
Swala ya Ijumaa kufuatia pia kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda yamekuwa ni matokeo ya vurugu watu kukimbizana
huku Polisi wakidhibiti Usalama na Amani kuelekea harijojo..
Maeneo ya Posta karibu na Wizara ya Mambo ya
Ndani Askari wameweka utepe wa kudhibiti watu kuingia katika maeneo hayo
kitendo kilichosababisha shughuli nyingi kusimama.
Pichani ni Jeshi la Wananchi Tanzania
likiwasilia maeneo ya Kariakoo kuongezea nguvu kwa ajili ya kutuliza ghasia.
Baadhi ya waumini
wanaodaiwa kutoka kikundi cha dini ya kiislamu wakidhibitiwa eneo la jirani na
geti la Ikulu..mapema leo ambapo jumla ya watu 6, walikamatwa.
Pichani ni maeneo ya Kariakoo magari ya
jeshi JWTZ zaidi ya 8 yakiwa katika doria maeneo ya Kariakoo.
No comments:
Post a Comment