Mtuhumiwa Pacficus akipelekwqa mahakamani chini ya ulinzi mkali |
JESHI
la Polisi mkoani Iringa, limeendeleza usiri mkubwa wa kumficha mtuhumiwa wa
mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten,
Daudi Mwangosi.
Ikiwa
ni mara ya tatu kwa mtuhumiwa huyo, Pasificus Cleophace Simon (23), kufikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi jana, ulinzi mkali ulitawala eneo hilo, huku
waandishi wakipigwa vikumbo wakizuiwa kupiga picha.
Askari
wenye sare wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) wakiwa na virungu, silaha za moto
huku wengine wakivalia kiraia, walitanda mahakamani hapo kuhakikisha hakuna
mwandishi anampiga picha mtuhumiwa huyo.
Katika
patashika hiyo, mwandishi wa habari wa gazeti la Majira, Eliasa Ally, alijikuta
akipigwa na askari ambao walikuwa wakimzuia kupiga picha.
Askari
aliyempiga mwandishi huyo alitambulika kwa jina moja la Idirisa, na hivyo tukio
hilo likazidisha uhasama baina ya jeshi hilo mkoani hapa na waandishi wa
habari.
Mtuhumiwa
huyo alifikishwa mahakamani akiwa amevalia jaketi lenye kofia iliyomfunika
kichwa kizima kiasi cha sura yake kutotambulika.
Akiwa
mahakamani hapo, wakili wa serikali ambaye pia ni mwendesha mashtaka ya
mtuhumiwa huyo, Lilian Ngilangwa, alimweleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Dyness
Lyimo, kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Lyimo
aliomba kesi hiyo ihairishwe hadi Novemba 7 mwaka huu itakapotajwa tena.
Pasificus
alifikishwa mahakamani hapo, akidaiwa kumuua kwa makusudi Mwangosi wakati wa
ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kijiji
cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa, mnamo Septemba 2, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment