Kanali Muamar Gaddafi |
Mwaka mmoja baada ya kukamatwa na
kuuwa kwa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi tarehe 20 mwezi Oktoba
mwaka 2011, familia yake iko wapi?
Watoto
watatu wa Gaddafi waliuawa wakati wa harakati za mapinduzi akiwamo aliyekuwa
mshauri wake wa usalama wa kitaifa Mutassim Gaddafi, aliyefariki mikononi mwa
waasi siku moja na babake.
Jamaa
za Gaddafi wanaosalia wamekumbwa na hali tata tangu kifo cha Rais huyo mwezi
Oktoba, huku mjane wake akitafuta hifadhi katika nchi jirani ya Algeria,
mwanawe na aliyeonekana kama mrithi wa wake Saif al-Islam yuko gerezani nchini
Libya akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake kuhusu uhalifu wa kivita.
SAFIYA GADDAFI (MJANE WA GADDAFI)
Safiya
Farkash, mama wa watoto wanane wa Gaddafi amekuwa akiishi nchini Ageria
alikopewa hifadhi kwa sababu za kibinadamu. Pamoja
na wanawe Ayesha na mwanawe wa kambo kutoka kwa mke wa kwanza wa Gaddafi,
waliingia nchini Algeria wakati waasi walipoudhibiti mji mkuu Tripoli. Amepewa
hifadhi nchini humo na kuwekewa vikwazo na serikali vya kutotoa matamshi yoyote
ya kisiasa wala kuingilia mambo ya Libya
MUHAMMAD GADDAFI (MWANAWE)
Ikiwa
mambo yangekwenda vinginevyo Muhammad angehudhuria michezo ya Olimpiki 2012
kama mkuu wa kamati ya michezo hiyo nchini Libya. Badala
yake, Muhammad mwanawe wa kwanza Gaddafi, amekuwa nchini Algeria kwa mwaka
mmoja sasa tangu kukimbilia huko wakati waasi walipovamia mji wa Tripoli.
Ni
mtoto wa mke wa kwanza wa Gaddafi, Fathia, pia alikuwa mwenyekiti wa kampuni ya
taifa mawasliano ya simu za mkononi nchni Libya. Hatakikani
na mahakama ya ICC na hakuhusika pakubwa na kujaribu kuzima harakati za
mapinduzi dhidi ya babake mwaka jana.
SAIF AL-ISLAM GADDAFI (MWANAWE GADDAFI)
Alionekana
na wengi kama ,mrithi wa babake, alikamatwa mwezi mmoja baada ya kifo cha
babake, na amekuwa akizuiliwa mjini Zintan tangu hapo. Alihitimu
kutoka chuo cha mafunzo ya uchumi mjini London, na amekuwa sababu ya mvutano
kati ya mahakama ya kimataifa ya ICC ambako anakabiliwa na tuhumza za uhalifu
wa kivita na maafisa wa sheria nchini Libya ambao wanasisitiza kuwa lazima kesi
yake iendeshwe nchini humo.
Idara
ya sheria nchini Libaya kwa sasa inaonekana kushinda katika mvutano huo, lakini
hakuna tarehe rasmi ya kusikilizwa kwa kesi yake, inaarifiwa kuwa jela ya
kifahari ikiwa na uwanja wa mpira wa vikapuni na mpishi wake binafsi
vimeandaliwa kwa Saif mjini Tripoli
SAADI GADDAFI (MWANAWE GADDAFI)
Saadi
Gaddafi, aliyekuwa mkuu wa shrikisho la soka nchini Libya pamoja na kuongoza
vikosi maalum, amepewa hifadhi nchini Niger ambako anaishi katika makao makuu
baada ya kutoroka kupitia jangwa la Sahara. Saadi
ana sifa tata ambapo alikuwa akicheza soka katika ligi ya Italia ingawa safari
yake ilikatizwa baada ya kuhusishwa na madawa haramu pamoja na maisha yake ya
anasa.
Niger
imekataa ombi la Libya kumpeleka nchini humo huku waziri wa sheria akisema kuwa
huenda akahukumiwa kunyongwa. Mnamo
mwezi Septemba, shirika la Polisi wa kimataifa Interpol lilitoa onyo ambalo
litawaruhusu nchi wanachama kamkamata Saadi.
Mwezi
Disemba mwaka jana polisi nchini Mexico walisema wana taarifa za kijasusi kuwa
magenge ya wafanyabiashara haramu ambao wanajaribu kumhamisha Saadi nchini
Mexico kwa kutumia stakabadhi bandia.
HANNIBAL GADDAFI (MWANAWE GADDAFI)
Hannibal
ni mtoto wa tano wa Gaddafi na Safiya Farkash. Inaamini alikuwa kwenye msafara
wa magari ya Gaddafi uliokuwa unaelekea nchini Algeria mwaka Jana .Alikuwa
anaongoza majeshi kulinda eneo la Gharyan, Kusini mwa Tripoli, kabla ya waasi
kudhibiti Tripoli.
Alisifika
kwa tabia zake za anasa na aliwahi kukamtwa akiwa amelewa wakati akiendesha
gari aina ya Porsche mjini Paris. Alizua
mgogoro wa kidiplomasia na Uswizi baada ya kuwashambulia wafanyakazi wawili wa
hoteli nchini humo na kusababisha babake kuwafunga jela wafanyakazi kutoka
nchini humo, na hata kuiwekea nchi hiyo vikwazo.
AISHA GADDAFI (MWANAWE GADDAFI WA KIKE)
Mwanawe
pekee wa kike alipewa hifadhi nchini Algeria pamoja na mamake na ndugu yake. Siku
tatu baada ya kuwasili Algeria, alijifungua mtoto msichana na kumuita Safiya,
jina la mamake.
Licha
ya kuwekewa ulinzi mkali na serikali ya Algeria, aliripotiwa hivi karibuni
kuwataka watu nchini Libya kupindua serikali ya sasa. Kwa usaidizi wa wakili
wake Muisraeli, aliitaaka mahakama ya ICC kuchunguza kifo cha babake
Aisha
pia aliripotiwa kuunga mkono Algeria katika mechi moja kati yake na Libya
akisema kuwa serikali mpya ya Libya haimwakilishi kivyovyote.
HANAA GADDAFI (MWANAWE WA KUASILIWA)
Kanali
Gaddafi alikuwa kwa muda mrefu akidai kuwa Hanaa aliuawa katika shambulizi la
Marekani mwaka 1986 wakati akiwa na mwaka mmoja na nusu. Lakini tangu mapinduzi
kufanyika, kumekuwa na taarifa kuwa Hanaa yuko hai ingawa hajulikani aliko.
MOUSSA IBRAHIM (ALIYEKUWA MSEMAJI WA SERIKALI)
Tarehe
20 mwezi Oktoba, mwaka mmoja baada ya kifo cha Gaddafi, taarifa kutoka kwa
ofisi ya waziri mkuu zilisema kuwa Ibrahim alikamatwa na waasi mjini Tarhouna,
maili arobaini kutoka mji mkuu.Maafisa wengine hata hivyo walishuku habari
hizo.Kumekuwa
na taarifa nyingi kuhusu kukamatwa kwake lakini baadaye ikasemekana kuwa uongo.
Alikuwa
mwsemaji wa serikali na kujulikana na vyombo vya habari vya kimataifa,
alionekana mwisho mjini Tripoli kabla ya waasi kuudhibiti mji huo.
Kila
siku alitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuwahakikishia kuwa serikali
itaendelea kuwa imara na kwamba waasi hawatafanikiwa kuiangusha.Alitoka kabila
moja na Gaddafi na alijigamba kuishi nchini Uingereza kwa miaka 15 kabla ya
kurejea nyumbani.
Habari kwa hisani ya BBC.
No comments:
Post a Comment