Iringa Urban Legislator, Hon. Rev. Peter Msigwa |
Akizungumza
kwa njia ya simu na mtandao huu Msigwa amesema mkutano huo unatarajiwa kuanza
kuanzia saa tisa alasiri katika uwanja wa mwembetogwa.
Amesema
kuwa ameamua kufanya mkutano huo ili kuweza kupata maoni toka kwa wananchi
kabla ya kurudi bungeni ili aweze kuwasilisha kero zao na kuwa ni njia mojawapo
ya kuweka uhusiano mzuri baina ya wananchi hao na mbunge huyo.
Ameongeza
kuwa katika mkutano huo atakuwepo mbunge wa Joshua Nasari "Dogo
Janja" kwaajili ya kuwapa hamasa vijana kufahamu demokrasia iliyo makini
na kila mtu kuitumia katika kufanya maamuzi katika jamii yake.
Amewataka
wananchi wa Jimbo la Iringa mjini na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi ili
waweze kupata fursa ya kueleza kero zao.
No comments:
Post a Comment