Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika
kitabu cha wageni mara baada ya kupokelewa katika Bunge la Seneti la Canada.
Kulia ni Spika wa Bunge hilo Mhe Noel Kinsella, anayefuatiwa na Waziri Mkuu wa
Canada Mhe Stephen Harper na Spika wa Bunge la wawakilishi la Canada (House of
Commons), Mhe Andrew Scheer pamoja na viongozi wengine wa bunge hilo Alhamisi
Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Spika wa
Bunge la Seneti la Canada ramani ya dunia na njia za meli, pamoja na
kuoneshwa chemba ya mikutano ya Maseneta wa Bunge la Canada Alhamisi
Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa Waziri Mkuu wa Canada
Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, Alhamisi
Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri
Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper wakitembea kuelekea kwenye chumba cha mkutano
kuongea na wanahabari. Zuria jekundu na bendera za Canada za kiongozi wa
nchi husika huwekwa sehemu hiyo kwa heshima na wakati wa ziara ya
kiongozi wa nchi ya nje aliye katika ziara rasmi nchini humo
Picha na IKULU
No comments:
Post a Comment