To Chat with me click here

Thursday, October 18, 2012

WATATU MBARONI MAUAJI YA BARLOW

Marehemu Kamanda Barlow
JESHI la Polisi Mkoani Mwanza, limesema linawashikilia watu watatu ambao wanahusishwa na mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, marehemu Liberatus Barlow.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Joseph Konyo ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RC0) Mkoa wa Mwanza, wakati akizungumza na vyanzo vya habari hii alisema kuwa, watu watatu wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo.

Alisema watu wanaoshikiliwa majina yao, yamehifadhiwa kwa ajili ya usalama, huku wakiendelea kuhojiwa.

“Tunachoshughulika nacho hivi sasa, ni kufanya mahojiano na kila mmoja ambaye kwa namna moja au nyingine, anaweza kutusaidia kumpata mhusika halisi wa mauaji hayo,” alisema …hutuwezi kumuonea mwananchi yeyote kuhusiana na tukio hili, hata hawa ambao tunawahoji kwa ajili ya kupata taarifa, wanapaswa kuwa na amani tu,” alisema Konyo.

Alisema jeshi la polisi, haliwezi kusema ni nani hasa ambaye alihusika na tukio hilo, kwa kuwa uchunguzi unaendelea.

Katika hatua nyingine, taarifa za uhakika toka ndani ya jeshi hilo, zinasema msako mkali umekuwa ukiendelea kila kona ya Jiji la Mwanza.

Taarifa zinasema, mbali na jeshi la polisi kumshikilia Doroth Moses tangu siku ya tukio, bado ni msaada mkubwa kwao.

Watu hao wawili ambao ni marafiki, wanashikiliwa kutokana na mtandao wa simu kuonyesha kuwa, kulikuwa na mawasiliano ya ujumbe mfupi wa simu ya mkononi juu ya mwenendo wa Doroth na Kamanda Barlow.

“Katika mojawapo ya ujumbe uliotumwa na mmoja wa marafiki wa mpenzi wa Doroth, ambaye naye anashikiliwa, ni ule ambao ulikuwa umkitaarifa kuwa, mwanamke aliye naye, amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na RRP Barlow, ambapo mpenzi huyo wa mwanamke aliyekuwa na Barlow, alijibu kuwa Mungu ndiye atakayelipiza juu ya tukio hilo,” kilisema chanzo toka ndani ya jeshi la polisi.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, watuhumiwa hao watatu wanashikiliwa na polisi na kuwekwa katika vituo vitatu tofauti, ili kuzuia mwingiliano wowote ambao unaweza kutibua uchunguzi.

Toa Maoni yako kwa habari hii

No comments:

Post a Comment