Wapiganaji
wa kiisilamu wanaodhibiti sehemu za Kaskazini mwa Mali, wanajipatia pesa kutoka
kwa biashara haramu ya mihadarati na kupitia kwa visa vya utekaji nyara ambapo wanalipwa
kikombozi ili kuwaachilia mateka. wakati
wakitumia sheria ya kiisilamu katika maeneo wanayodhibiti.
Madai
haya ni kwa mujibu wa afisaa mmoja mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Wapiganaji
hao pia wananunua watoto kuwatumia kama wanajeshi, huku wakilipa familia za
watoto hao dola mia sita kwa kila mtoto. Alisema Ivan Simonovic baada ya kuzuru
nchi hiyo.
Wapiganaji
hao wenye siasa kali, walitwaa thuluthi mbili za udhibiti wa Mali, wakati nchi
hiyo ilipotumbukia katika vita baada ya kufanyika mapinduzi ya kijeshi. Bwana
Simonovic alitoa picha ya kutisha kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu
unaofanyika katika eneo hilo.
''Haki
za wanawake hasa zinakiukwa pakubwa'' alisema afisaa huyo ambaye ni naibu wa
katibu mkuu kuhusu haki za binadamu katika Umoja wa mataifa ,akielezea kuhusu
orodha ya wanawake ambao hawajaolewa au wale ambao walikuwa wamepata watoto.
Wanawake
zaidi wanalazimishwa kuolewa huku gharama ya kupata mke ikiwa dola elfu moja.
''Visa
vya ukiukwaji wa haki za binadamu hapa ni vya kushtua na vinafanyika sana''
aliambia waandishi wa habari mjini New York, akiongeza kuwa wapiganaji hao
wanatumia sheria kali za kiisilamu kudhibiti eneo hilo.
Katika
ziara ya afisaa huyo ambayo ilinuia kugundua yanayoendelea nchini Mali,
aligundua kuwa wapiganaji hao wanatumia sheria kali kwa wahalifu. Hadi
kufikia sasa, watu watatu wamenyongwa hadharani na wengine wanane kukatwa
mikono huku wawili wakichapwa hadharani.
No comments:
Post a Comment