To Chat with me click here

Thursday, October 11, 2012

NYERERE AWAONDOA HOFU WAPIGA KURA


Mhe. Vicent Nyerere

MBUNGE wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (CHADEMA), amewaondoa hofu wananchi wa jimbo hilo, kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa na Chuo Kikuu cha Wauguzi iliyopo jimboni humo na kusema miradi hiyo ipo mbioni kuanza kutekelezwa.

Nyerere alisema hayo juzi alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, uliofanyika kwenye viwanja vya Nyakato Shuleni mjini Musoma na kuongeza kuwa taratibu zote za kuanza ujenzi wa miradi hiyo imeshakamilika, kwani tayari wataalamu wa kusimamia ujenzi huo wameshafika mjini Musoma.

“Ujenzi wa hospitali yetu ya Rufaa ya Kwangwa na kile chuo cha Uuguzi ipo mbioni kuanza kujengwa. Taratibu zote za ujenzi zimeshakamilika na juzi juzi hapa wataalamu walifika kwa ajili ya upimaji tayari kwa utekelezaji wa kujengwa miradi hii ya maendeleo.“Lakini, natumia mkutano huu kuwaonya wana CCM wanaowapotosha wananchi kwamba eneo la hospitali na chuo hicho wamepewa wawekezaji. Huo ni uzushi na uongo mtupu. Siasa na uongo zisiwepo kwenye maendeleo, ni bora tutaniane sehemu nyingine, lakini isiwe kwenye maendeleo,” alisema.

Kwa upande mwingine, Nyerere aliwahakikishia wafanyakazi wa Kiwanda cha nguo cha Mutex kulipwa fidia zao, kwani alishazungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, kuhusu kulipwa wafanyakazi hao na kwamba waziri huyo alihidi bungeni kwamba serikali itawaongezea fedha za fidia tofauti na ilivyowalipa awali.

No comments:

Post a Comment