To Chat with me click here

Wednesday, October 31, 2012

HIVI NDIVYO MOSHI ILIVYO LEO!!!

 Baadhi ya Maeneo ya Mji wa Moshi kama yaonekanavyo yalivyo masafi.
Haya ni maeneo ya Stendi Kuu ya Mabasi-pamoja na kuwa na pirikapirika nyingi lakini bado usafi ni wahi ya juu

Moshi ni moja kati ya miji misafi katika Afrika ya Mashariki, usafi wa mji huu wa Moshi umekuwa ukiibua mjadala na maswali mengi sana kichani kwangu na kwa baadhi ya watanzania wenye kudadisi mambo. 

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kuutembelea huu mji katika moja ya shughuli zangu, na nilipokuwa nikipita katika baadhi ya maeneo ya mji huo, kwakweli nilishuhudia ni jinsi gani wakaazi wa manispaa hiyo walivyojidhatiti katika kuhakikisha waufanya mji wao kuwa msafi na mfano wa kuigwa katika Tanzania yetu na hata nje ya mipaka yake. 

Maswali mengi ambayo nimekuwa nikijiuliza ni kuwa; 
  1. Hivi watanzania wa mikoa mingine hususani Dar-Es-Salaam, hawaoni umuhimu wa kutunza mazingira na kudumisha usafi wa jiji kama ilivyo kwa manispaa ya moshi? 
  2. Je watu hawa wa moshi si watanzania kama sisi wa mikoa na sehemu nyingine za Tanzania? 
  3. Kama ndivyo je ni kwanini tumekuwa na utofauti wa kiutashi katika kujali na kutumnza mazingira? 
  4. Vipi kuhusu viongozi wa halmashauri nyinginezo pamoja na serikali kuu? Je hazipaswi kuiga mfano wa manispaa ya moshi, viongozi wetu hususani wa hapa Dar, wamekuwa wakipigapiga maneno tuu juu ya utunzwaji wa mazingira lakini hakuna hatua thabiti zinazochukuliwa pale watu wanapothibitika kuvunja sheria nyingi za kimazingira. 
  5. Pia kwa dhana hii ya uchafu uliokithiri katika miji na vitongoji vyetu, je tunaweza kutekeleza kwa dhati azimio la serikali la kupambana na magonjwa ya milipuko kama maralia, kipindupindu n.k ? 
Maoni yangu: 

Kwanza kwa dhati ya moyo wangu napenda kuwapongeza sana viongozi wa manispaa ya Moshi kwa kuwajibika ipasavyo na kuhakikisha utekelezwaji wa mipango na malengo yao ya kuifanya moshi kuwa mfano wa kuigwa kiusafi. 

Napenda pia kuwashukuru wananchi wa Manispaa hiyo ya Moshi kwa kuwa waelewa na wenye kutambua umuhimu wa kutunza mazingira na kudumisha usafi wa mji wao kiasi ya kuupa heshima kubwa katika Tanzania yetu na kuwa mfano wa kuigwa. Ninawapongeza sana kwa utiifu wa sheria zao na kwa kuzitekeleza bila shuruti. 

Nawaasa viongozi wa halmashauri na manispaa nyinginezo; kuwa wabunifu wa mbinu mbalimbali ambazo zitasaidia kutoa hamasa kwa wananchi wao kudumisha usafi wa mazingira yetu kwam ilivyo moshi. 

Viongozi hawa, pia wao wenyewe wawe ni mfano bora wa kuigwa katika kutekeleza maazimio ya kimazingira. Wawe tayari kusimamia na kuwajibika pia kuwawajibisha wahusika wote ambao ni kikwazo kwa kufikia au kutekeleza malengo mazuri ya kudumisha usafi wa mazingira yetu katika halmashauri zetu. 

Wananchi wote kwa ujumla, tunapaswa kuelewa kuwa usafi ni moja ya njia muhimu za kupunguza ugumu wa maisha haswa kwa sisi wananchi wenye kipato cha chini. Tukumbuke kuwa magonjwa mengi hutokana na uchafu, haya magonjwa huongeza gharama kubwa mno katika maisha, kwani pesa nyingi huitajika katika kujitibu. 

Pia sisi kama watu na taifa linaloendelea kukua kiuchumi, kimazingira, kijamii na kitekenologia basi si vyema tukabaki nyuma katika suala zima la usafi. Ni wajibu wetu na wa kila mwananchi kutunza mazingira yake. Hili pia linaweza kusaidia kupunguza pesa nyingi zinazopotea katika kutunza mazingira ambayo kila mmoja wetu anawajibu huo. 

Ni matumaini yangu kuwa kwa waraka huu mfupi, kila mmoja wetu atakayepata nafasi ya kuupitia, atafahamu nini umuhimu wa usafi na kwanini nimekuwa nikiunga mkono harakati za wana-Moshi katika kutunza na kudumisha usafi wa manispaa yao. 

Mtanzania Badilika Sasa!!!  

No comments:

Post a Comment