POLISI
wilayani Arumeru inamshikilia Kada wa CCM, Edward Simon maarufu kama Bosco kwa
tuhuma za kumtishia kwa bastola mfuasi wa Chadema.Kada huyo wa CCM, anatuhumiwa
kutishia kumuua kwa kumpiga risasi mfuasi wa Chadema, Boniface Kimario
aliyekuwa akipita mitaani kutangaza mkutano wa hadhara wa chama chake
uliotarajiwa kufanyika eneo la Sasi.
Hatua
ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ilikuja baada ya aliyetishiwa kufungua jalada
la malalamiko Kituo cha Polisi cha USA-River na kupewa namba ya mashtaka
USR/RB/4245/2012, kosa la kutishia kuua kwa silaha.
Mtuhumiwa huyo aliyewekwa rumande baada ya kufikishwa kituoni hapo na polisi aliyekuwa akitumia usafri wa pikipiki.
Mratibu
wa Kampeni za Chadema katika kata hiyo, Henry Kileo alisema wakati akitishiwa
kuuawa kwa kupigwa risasi, Kimario alikuwa akitekeleza jukumu la kutangaza
mkutano wao wa hadhara na baadaye kwenda kumfuata mgombea wa Chadema, Peter
Msere nyumbani kwake Kijiji cha Bangata.
Kileo
alisema wakati Kimario aliyekuwa kitumia gari aina ya Range Rover, ghafla
mtuhumiwa alijitokeza na kuziba barabara kwa kutumia gari lake ndogo aina ya
Rav 4 na kuchomoa bastola, kabla ya kutishia kumpasua kichwa kwa risasi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas alisema hajapa taarifa hizo, kwa
sababu bado suala hilo linashughulikiwa na polisi wilayani Arumeru na kuahidi
kufuatilia.
Mkoa
wa Arusha unafanya chaguzi ndogo katika kata mbili za Bangata, Arumeru na
Daraja II mjini Arusha ikiwa ni kati ya kata 28 zinazofanya chaguzi ndogo,
baada ya nafasi hizo za udiwani kubaki wazi kutokana na sababu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment