To Chat with me click here

Monday, October 8, 2012

MJANE WA MAREHEMU DAUDI MWANGOSI AKANUSHA KUHUSU HABARI ILIYOANDIKWA KATIKA GAZETI LA HABARI LEO

Mhe. Msigwa akiwa na Aneth Mwangosi nyumbani kwake
Mjane wa marehemu mwangosi, Aneth Mwangosi ajibu shutuma za kile yaliyoandikwa Katika gazeti la Habari Leo toleo la Tarehe 05/10/2012 kuna habari inayomnukuu mjane wa Marehemu Mwangosi akimlaumu Dkt. Slaa na CDM kuwa ameshindwa kutimiza ahadi yake ya rambirambi na hata msaada wake wa kusomesha mmoja wa mtoto wa Marehemu Mwangosi.

Akizungumza hayo wakati akihojiwa na chombo kimoja mjini hapa (Iringa) nyumbani kwake asubuhi hii kwa masikitiko makubwa ameshangazwa kuona kile kilichoandikwa katika gazeti la Habari leo na kusema si kweli kwani yale aliyojibu si hayo yaliyoandikwa.

Mjane anaeleza kuwa Dr. Slaa hakuahidi rambirambi bali aliahidi kumsomesha mtoto wake wa pili ambaye amemaliza darasa la saba. Ambaye kwa sasa ameanza kupata masomo ya Tuition ambapo msaada huo umetolewa na mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa ambaye ni jirani yake.

Mjane wa marehemu ameeleza kuwa kutokana na habari hiyo amekuwa akipata shida sana kwani ndugu zake wamekuwa wakimpigia simu na kumlaumu kutokana na upotoshwaji katika habari hiyo.

Pia amewashukuru wote walioshikiana nae katika msiba wa marehemu mumewe Daudi Mwangosi na kueleza kuwa ushirikiano ulioneshwa mwanzo wazidi kuonesha.

 Mbunge Msigwa akihojiwa ameeeza "kuwa njaa ya siku moja isimfanye mwanahabari yeyote kuvunja maadili na kuandika habari zinazopotosha na kuleta madhara kwa jamii" na kuwataka wanahabari wote kuzingatia maadili yao ya kazi ili kuleta maendeleo na mabadiliko katika jamii.

No comments:

Post a Comment