Habari za leo kutoka Hospitali ya
Muhimbili zinadai hali ya mtoto Juliana Mwinuka kwa jana na leo imekuwa
ya kutia matumaini baada ya kuanza kula na kunywa dawa na hata kuomba
chakula anachokitaka ,pia jicho lake moja limeanza kuonyesha dalili
ya kupona huku tatizo kwa sasa miguu yake hainyoki na yawezekana
akaanzishiwa mazoezi zaidi .hizi ndizo habari mpya juu ya Juliana
Mwinuka.
Mtandao huu wa Maxmillian Kattikiro unaendelea kuwapongeza wote wanaoendelea
kuguswa na kuungana na wadau wengine kumchangia fedha za matibabu ,mtoto
Juliana kama anavyoonekana akiwa ameunga uso wake kwa moto ni yatima anahitaji
msaada wako ili kunusuru maisha yake waweza kutuma mchango wako kwa njia ya
M-PESA katika namba hii 0754 026 299 au Tigo Pesa 0712 750199 namba hizi ni za
mmiliki wa mtandao wa Francis Godwin
Usikose kuendelea kufuatilia blog hii, ili kuona picha zaidi za maendeleo ya mtoto Juliana.
No comments:
Post a Comment