Women in Balance Director - Dina Marios |
Mkurugenzi wa Women in
Balance Dina Marios akizungumza na wageni waalikwa kufafanua hatua ya awali ya
maandalizi ya kufanyika kwa tukio la mafunzo ya‘Kitchen Party
Gala’ kwa kina mama jinsi ya kuishi ndani ya ndoa ili kujenga
familia bora litakalofanyika mnamo tarehe 21 mwezi huu.
Akifafanua zaidi amesema
tukio hilo la 4 litakalokuwa la mwisho kwa mwaka huu litakalofanyika kuanzia
saa 8 mchana mpaka saa 4 usiku litafanyika katika hali ya ubora zaidi katika
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Aidha amewataka wanawake
kuhudhuria kwa wingi ili waweze kupata faida kwa ajili yao binafsi na kuweza
kuwa waalimu bora kwa waume zao jambo litakalosaidia kuepusha migogoro ya mara
kwa mara inayopelekea kuvunjia kwa ndoa.
Wadhamini wa Kitchen
Party Gala ni TSN Super Market, Sossi, Coca Cola na Clouds Fm.
Mahali:Diamond Jubilee
VIP hall Muda:Kuanzia saa nane mchana mpaka saa nne usiku. Kiingilio ni
Tsh 30,000 Ukitaka kubook meza ya watu kumi piga
namba 0787583132,0716485666 Safarii hii ukiacha wasemaji kuna burudani ya
kila aina ukizingatia ni ya mwisho kabisa kwa mwaka huu.Bila kusahau chakula,na
vinywaji laini.
RANGI YA
SIKU.
Kwa muda kina dada/mama
mmekuwa mkitoa maoni mnataka kushona nguo mtokelezee. Basi rangi ya siku ni rangi ya chenza (tangerine tango)color of the year
2012. Ishone utakavyotaka wewe
iwe kitambaa cha kawaida,kitenge,kanga,batiki,au ukachanganya vyovyote ili
mradi uzingatie rangi ya siku.
No comments:
Post a Comment