Wakati
magari 150 ya msafara wa ziara ya Rais Barack Obama yamewasili nchini, majina
ya mawaziri wa Tanzania yatakayoruhusiwa kumpokea kiongozi huyo kuchujwa na
makachero wa FBI.
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Moses Malaki aliliambia gazeti hili jana kuwa matayarisho ya ujio wa Rais huyo ni kabambe na hayajawahi kutokea katika historia ya Tanzania.
Pia
alisema shughuli za kumpokea Rais Obama, anayetarajiwa kutua Jumatatu saa 8:40
mchana, zitaanza asubuhi kwa maofisa wa Marekani kushika majukumu yote katika
uwanja huo, ikiwemo kuongoza ndege, ukaguzi wa abiria na mizigo, kwa maana
wafanyakazi wa uwanja huo kuwa likizo kwa siku mbili.
“Wamesema
kuwa wao watasimamia kila kitu kuanzia wageni watakaoingia na kutoka na wataamua
nani aingie na kutoka,” alisema Malaki.
Aliongeza kuwa japokuwa Mamlaka ya Anga Tanzania (TAA) inaendelea kufanya kazi zake kama kawaida, lakini Jumatatu, Wamarekani watasimamia kila kitu hadi ukaguzi wa wageni.
“Siku
hiyo mwongoza ndege wa TAA, atafanya shughuli kidogo, mambo mengine yatafanywa
na wao,” alisema.
Idadi ya maofisa wa Tanzania
Imebainika
kuwa hata idadi ya maofisa wa Tanzania wakiwemo viongozi watakaompokea pia
itapangwa na Wamarekani wenyewe.
“Wenyewe
wana orodha yao na wanajua nani atakuwepo au hatakiwi kuwepo katika kundi la
wageni watakaompokea Rais Obama,” alisema na kuongeza:
“Nilimuuliza
Ofisa Usalama wa Marekani iwapo nitaweza kumwona Rais Obama, akaniambia:
Utamwona ukibahatika kuwepo kwenye orodha.”
Waziri
wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe naye alikiri kuwa mawaziri wanaotakiwa
kuwepo katika msafara wa kumpokea Rais Obama ni wachache watakaochaguliwa tu na
Wamarekani, baada ya kuyapitia na kuyachunguza majina hayo kwanza kabla ya
kuyakubali.
“Hii
sijawahi kuiona, hata sisi wenyewe tunateuliwa na wakishayapitia wataamua, nani
aende au asiende,” alisema Chikawe.
Mwananchi
Mwananchi
No comments:
Post a Comment