Kampuni
kubwa ya mafuta ya Shell inatarajiwa kufikishwa mahakamani leo nchini Uholanzi,
ikikabiliwa na mashtaka ya kuchafua mazingira katika vijiji kadhaa nchini
Nigeria. Kesi
hiyo imewasilishwa mahakamani na wakulima wanne wa Nigeria kwa ushirikiano na
shirika moja la kutetea mazingira la nchini humo, Friends of the Earth.
Ni
mara ya kwanza kwa kampuni kubwa ya Uholanzi inashtakiwa katika mahakama ya
kiraia nchini humo kuhusiana na uharibifu uliotokea katika nchi ya kigeni. Shell,
inasisitiza kuwa haijaweza kusafisha eneo ambalo lilichafuka kutokana na
shughuli zake nchini Nigeria. Inasemekana
kuwa nusu ya uvujaji wa mafuta katika eneo hilo imesababishwa na visa vya wizi.
Kesi
hiyo inahusishwa na uvujaji wa mafuta uliotokea katika eneo la Ogoniland nchini
Nigeria. Wakulima
wanasema kuwa mafuta yaliyovuja kutoka kwa mabomba ya mafuta ya kampuni hiyo,
yameathiri mapato yao, kwa kuharibu mimea na mabwawa ya samaki.
Mmoja
wa walioshtaki kampuni hiyo, Alfred Akpan, aliambia BBC kuwa mafuta yaliyovuja
yaliharibu vibaya mabwawa yake 47 ya samaki na anataka fidia.
No comments:
Post a Comment