Uganda inatishia kujiondoa katika
mazungumzo ya kuleta amani katika nchi kadhaa barani Afrika.
Tisho
hilo linafuatIa ripoti ya Umoja wa mataifa iliyokashifu Uganda kwa madai ya
kuunga mkono makundi ya waasi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Waziri
wa serikali , Asuman Kiyingi, alisema kuwa dhana kuwa Uganda inaunga mkono
waasi wa M23 katika DRC wakati ikiwa mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya amani
ni njama ya kuidhalilisha na kuiharibia sifa nchi hiyo.
Aliongeza
kuwa , ikiwa madai hayo hayataondolewa dhidi yake pamoja na juhudi za nchi hiyo
kukosa kutambulika, serikali itaondoa wapatanishi wake kwenye mazungumzo ya
amani.
Amesema
pia vikosi vya nchi hiyo vilivyo nchini Somalia na Jamuhuri ya Afrika ya Kati,
pia vitaondolewa.
Vikosi
hivyo vinaungwa mkono na Umoja wa Mataifa hatika harakati zao dhidi ya waasi na
wanamgambo.
No comments:
Post a Comment