To Chat with me click here

Friday, October 12, 2012

CHADEMA WASISITIZA NCHIMBI ANG`OKE

Mhe. Vicent Nyerere
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeng’ang’ania Waziri wa Mambo ya Ndani, Emanuel Nchimbi, afukuzwe kazi kutokana na kushindwa kusimamia haki na usalama wa raia nchini.

Tamko hilo limetolewa na Mbunge wa Msoma Mjini (Chadema), Vicent Nyerere wakati akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku mbili tu baada ya Kamati aliyoiunda Nchimbi kumaliza kuwasilisha ripoti yake kuhusu mauaji ya aliyokuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoani Iringa, Daud Mwangosi.

Nyerere akizungumza kwa niaba ya Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema waziri Nchimbi anapaswa kuwajibishwa kutokana na matumizi mabaya pesa za umma kutokana na kuunda kamati, ambayo imeshindwa kubaini ukweli wa tukio la mauaji ya Mwangosi.

Alisema kitendo cha waziri huyo kupokea ripoti ya kamati hiyo yenye utata inaonyesha wazi kuwa, Serikali haina nia njema ya kukemea mauaji ya raia yanayotokea kwenye maandamanao na mikutano ya kisisasa.

“Kamati ya Nchimbi ilikuwa na lengo la kulisafisha jeshi hilo, huku mazingira ya tukio lenyewe likionyesha wazi kuwa  polisi walihusika kwa asilimia zote sijui  anakwepa nini,”alihoji Nyerere.

Nyerere alisema kuwa bunge lililopita  aliwasilisha hoja ya kupitishwa kwa sheria kunapotokea mauaji yenye sura ya kisiasa  uchunguzi ufanywe wa kimahakama ili kuwachukulia hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment