Wagombea Mit Romney na Barack Obama wakielezea sera zao za kigeni |
Rais wa Marekani Barack Obama na
mpinzani wake wa Republican Mitt Romney wametofautiana kuhusu sera ya kigeni ya
Marekani katika mdahalo wao wa mwisho wa runinga kabla ya uchaguzi ujao wa
Urais.
Romney alimlaumu Rais Obama kwa
kushindwa kutoa uongozi unaofaa kwa dunia na ameruhusu amani mashariki ya kati
kuvurugika.
Hata hivyo Obama alimkosoa Romney
akisema amekuwa akipinga sera zote kuu za marekani ikijumuisha kuivamia Iraq.
Wagombea hao wamezungumzia sana kuhusu
swala tete la harakati za mageuzi katika nchi za kiarabu,sawa tete la ran,
Israel na China.
Bwana Obama alisema mpinzani wake hana
uelewa kuhusu sera ya kigeni lakini Romney naye akamwambia kuwa ameruhusu
vurugu kukumba Mashariki ya kati.
Kura za maoni zilizotolewa punde baada
ya kukamilika mjadala huo, zilionyesha Obama kuwa mshindi.
Mjadala huo uliofanyika katika chuo
kikuu cha Boca Raton, haukuwa na ubishi kama mjadala wa pili wiki jana ambapo
rais Obama alijitokeza kisabuni kuonyesha wapiga kura kuwa ye ndiye kiongozi
anayestahili kuchaguliwa mwaka ujao.
Lakini ubishi ulijitokeza mara kwa mara
hasa ambapo Obama alitaka kuonyesha wapiga kura kuwa Mit Romney hana uelewa
mzuri kuhusu sera ya kigeni na kwamba hawezi kuwa kiongozi mzuri.
No comments:
Post a Comment