To Chat with me click here

Friday, October 12, 2012

CHADEMA WAIPIGIA KURA CCM

UCHAGUZI wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, ulikumbwa na mvutano mkali kati ya vyama viwili vya upinzani, hali iliyosababisha mgombea wa CCM kushinda uchaguzi huo.

Uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashari hiyo, ambapo mgombea wa CCM, Evarist Momburi alishinda kwa kupata kura 24 kati ya 44, huku mgombea wa Chama cha Tanzania Labour, (TLP), akipata kura 17.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya kutokea mvutano mkubwa baina ya vyama vya TLP na Chadema, kutokana na TLP kusimamisha mgombea, kinyume na makubaliano, ambapo awali inadaiwa vyama hivyo viliafikiana Chadema isimamishe mgombea.

Kutokana na hali hiyo, mgombea wa Chadema, Alex Umbela ambaye ni Diwani wa Kata ya Kirua Vunjo Mashariki, alitangaza kujitoa katika kinyang’anyiro hicho na kumwacha mgombea wa CCM, Evarist Momburi akipambana na Jese Makundi wa TLP.

Katika kinyang’anyiro hicho, mgombea wa CCM alishinda baada ya madiwani wa Chadema kuonekana kumuunga mkono, ili kumwangusha mgombea wa TLP, ambaye alikuwa anagombea nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.

Akizungumza wakati wakujitoa katika kinyang’anyiro hicho, mgombea wa Chadema Alex Umbela, alisema amefikia uwamuzi huo ili kulinda heshima ya chama chake.

Akizungumza katika uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Moris Mkoi aliwataka watendaji wa halmashauri hiyo kwenda vijijini, ili kusikiliza kero za wananchi.

No comments:

Post a Comment