![]() |
Lakini
hivi karibuni hautahihajika kupanda gorofa kutafuta gari lako kwani kampuni ya
kutengeza magari ya BMW, imetangaza kuzindia kifuaa ambacho kinaweza
kuyawezesha magari ya kampuni hio kujiegesha yenyewe kwa kubonyeza tu kifaa
hicho.
Hata
hivyo dereva wa gari hilo atalazimika kuvaa saa ya Smartphone mkononi ambayo ataibonyeza
na kuiamrisha kwa sauti gari hilo kwenda kujiegesha.
Gari
hilo kwa amri ya dereva litatoka liliko baada ya dereva kushuka na kwenda
lenyewe kwa kuhesabu muda utakalichukua kwenda kutafuta sehemu ya kujiegesha.
Tawi
la kampuni ya BMW mjini Munich, Ujerumani limezindua teknolojia hio ambayo
inawezesha gari kujiegesha lenyewe.
Gari
hilo linatumia miale ya Leser iliyo kujitafutia ramani ya jengo ambalo lipo.
Dereva anaweza kuliamrisha gari hilo kwenda kujiegesha kwa kutumia Smartphone.
![]() |
Teknolojia
hio inajulikana kama ' Remote Valet Parking Assistant,' na inafanyiwa majaribio
kwenye gari la BMW i3.
Badala
ya kutumia GPS, teknolojia hio inatumia miale ya Laser ambayo hutengeza ramani
inayolisaidia gari hilo kutafuta sehemu ya kwenda kujiegesha.
Teknolojia
hiyo inaiwezesha gari hilo kuona njia na nafasi ya kujiegeshea na pia kuona
vizingiti mfano kama magari ambayo hayajaegeshwa vyema. Kwa
mujibi wa waliotengeza gari hilo, linaweza kujitafutia nafasi ya kujiegesha na
hata kuweza kutambua sehemu ambako kuna nafasi.
Teknolojia
hio inatengezwa sambamba na teknolojia nyinginezo zitakazoweza kuzuia gari hilo
kugongana na magari mangeine.
No comments:
Post a Comment