Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akikagua gwaride rasmi katika viwanja vya jumba la Rideau Hall jijini Ottawa,
Canada, katika hatua yake ya kwanza ya ziara rasmi ya siku mbili jijini
humo Jumatano Oktoba 4, 2012. Jumba hilo ndilo makazi na ofisi
rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangia mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi
humo pia hapo ndipo hutumika kwa kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya
vyema, pa kupokelea wageni mashuhuri wa nchi za nje na pia ndipo anapofanyia
shughuli zote za kitaifa akiwa kama mwakilishi wa Malkia wa Uingereza.
No comments:
Post a Comment