KIONGOZI
WA UPINZANI NCHINI VENEZUELA HENRIQUE CAPRILES AMEVUTIA UMATI MKUBWA WA WAFUASI
KATIKA KAMPEINI YAKE YA MWISHO YA UCHAGUZI MKUU MJINI CARACAS.
Wafuasi wa Kiongozi wa Upinzani Mjini Caracas. |
Bwana
Capriles , alimkosoa Rais Hugo Chavez kwa kile alichokiita orodha ndefu ya
ahadi ambazo hajawahi kutimiza. Aidha
alidai haki kwa wanaharakati watatu wa upinzani waliouawa wakati wa maandamano
katika jimbo la Barinas siku ya Jumamosi.
Bwana
Capriles alihutubia umati mkubwa wa wafuasi wake katika jimbo la Zulia akiahidi
kuendeleza mfumo wa ujamaa ikiwa atachaguliwa kwenye uchaguzi utakaofanyika
tarehe 7 mwezi huu.
Melfu
ya watu walifurika kwenye barabara za mji mkuu Caracas siku ya Jumapili,
kumuunga mkono bwana Capriles. "nadhani
huu ni mkutano mkubwa wa hadhara kuwahi kushuhudiwa mjini Caracas "
alisema bwana Capriles.
Bwana
Chavez pia aliwavutia maelfu ya wafuasi katika jimbo la Zulia. Ghasia zilikumba
kampeini hizo cha uchaguzi mkuu huku kukitokea vifo vya watu watatu siku ya
Jumamosi.
Rais
Chavez amewatahadharisha wananchi kuwa ikiwa upinzani utashinda uchaguzi huo ,
nchi hiyo huenda ikarejea nyuma miaka 30. "Mimi
sijawadanganya wala sijakosa kuwatimizia mahitaji yenyu," alisema rais
Chavez.
Kumekuwa
na visa vingine vya vurugu na ghasia wakati huu wa kempeini za uchaguzi.
Wafuasi wa pande zote mbili walirushiana mawe mapema mwezi Agosti, wakati bwana
Capriles alipojaribu kupita katika mji wa Puerto Cabello.
Huku
wasiwasi mkubwa kwa wapiga kura ukiwa uhalifu sugu, mwandishi wa BBC Sarah
Grainger, anasema kuna hofu ghasia zaidi huenda zikalipuka katika kile
kinachosemekana kuwa uchaguzi ambao umekuwa na ushindani mkali sana .
Bwana
Chavez amekuwa mamlakani tangu mwaka 1999, na aligundulika kuwa na saratani
mwaka jana.
Zaidi
ya vyama thelathini vya upinzani, vimemuunga mkono bwana Capriles.
Nini
maoni yako kuhusu uchaguzi mkuu nchini Venezuela? Je unahisi rais Chavez
ametawala vya kutosha?
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment